Bukobawadau

UWANJANI KAITABA MBEYA CITY FC YAIBAMIZA KAGERA SUGAR 1-0 LEO JUMAMOSI JAN 25,2014

 Uwanjani kaitaba leo Jumamosi Jan 25,2014 tinu ya MBEYA City imeendelea kufanya kile ambacho  hakuna timu ya mkoani iliwahi kufanya katika miaka kumi iliyopita kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Kwa kuendeleza ubabe wake katika uwanja wa ugenini, ambapo imewabamiza timu ya Kagera Sugar bao 1-0.
 Waamuzi wa Mchezo huu.
 Waamuzi wa mchezo huu katika picha ya pamoja na makaptain wa timu zote mbili.
Kikosi kamili cha Wachezaji wa Mbeya City.
Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi
Kizaa zaa langoni mwa Kagera Sugar kilicho pelekea mlinda mlango kuumia.
 Hekaheka katikati ya uwanja.
 Timu ya Kagera shuga ikijaribu kutafuta bao,Inakua ngumu kutokana na  kiwango kizuri cha mabeki wa Mbeya City, pichani ni sehemu ya hekaheka langoni mwa Mbeya City.
 Mwamuzi wa mchezo huu akijiandaa kutoa kadi ya njano kwa mchezaji wa Mbeya City.
Taswira uwanjani mchezo ukiendelea.
 Mchezaji Marley wa Kagera Sugar anaumia  mnamo dakika ya 70 kipindi cha pili
 Hapa anaonekana akitibiwa Jeraha.
Baada ya kutibiwa Jeraha , mchezaji Marley anaendelea kukipiga uwanjani.
 Benchi la Kagera Sugar katika sintfahamu.
Sehemu ya mashabiki uwanjani.
Bango la mashabiki wa Mbeya City.
Hamsha hamsha za mashabiki wa Mbeya City waliotokana na mchanganyiko wa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mjini hapa.
 Kocha  wa Kagera Sugar akitoa mawaidha kwa wachezaji wake.
 Hivi ndivyo dhahama ilivyo washukia wakata miwa wa Kagera Sugae.
 Wachezaji wa mbeya City wakishagilia bao.
 Jina la mfungaji linapatikana hivi punde.
Mashabiki wa Mbeya City Fc. wakifanya yao!
 Mashabiki wa Mbeya City wakizunguka uwanja mzima kwa shangwe.
 Mashabiki wa Kagera Sugar, wakiwa hawana maneno kabisa.
 Hali ni tete kwa mashabiki wa Kagera Sugar.
 Yusuph Abeid mtangazaji 88.5 Kasibante Fm Radio pichani kushono,kulia ni Mr Mpangala.
 Kutoka kushoto ni Said Mushamu,Didas Zimbihile, Yahya wakiteta na CTO.Willy Kiroyera.
 Kijana Sajidu, shabiki mkubwa wa Kagera Sugar .
 Mdau Salum Bonge, Patrick Pombe na Said Bunduki wakifuatilia soka linavyo endelea.
 Matokeo  mpaka mwisho wa mchezo yamesimama hivi( 1-0)
Mdau Shahidu  Sokwala na Hashimu wakiendelea kufuatilia soko.
 Baada ya mashine za ELECTRONIC kugoma,wadau waliendelea kukomaa na utaratibu wa siku zote
Mr Kijigo akitoa updates kupitia mtandao wakati soka linaendelea.
 Mashabiki jukwaani.
 Naona panatatizo pale na Redcross wanaingia Uwanjani

  Timu ya Mbeya City wakiongozwa na Antony Matogolo, Steven Mazanda na Deus Kaseke
 Kulia ni Mshambuliaji wa Kagera Sugar mwenye magoli 7 kwa sasa, Themi Felix
 Jukwaa la wagadi ni kimya baada ya Kagera kuwa nyumba kwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City
 Mlinda mlango wa Timu ya Kagera Sugar.
 Muonekano  wa uwanja wa kaitaba

Mbeya City wameendelea kuonyesha upinzani wa hali ya juu kwa kutofungwa na timu yoyote zikiwamo timu vigogo za Yanga, Simba na Azam.





Next Post Previous Post
Bukobawadau