Bukobawadau

BONANZA LA JOGGING & GLOBAL BREAKING NEWS LAFANA NDANI YA DAR LIVE

Washiriki wakimalizia mbio zao kutokea Uwanja wa Taifa mpaka Ukumbi wa taifa wa Burudani wa Dar Live.
Klabu mwenyeji, Kejo Community wakiwa jukwaani wakicheza kwa furaha katika Bonanza hilo.
Msanii wa Msondo Music Band, Hassan Moshi (mwenye Mic) akikosha nyoyo za wana Jogging waliohudhuria kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News leo.
Timu ya klabu ya Jogging ya Magenge 20 wakipepetana na Spurs (jezi nyeupe) katika mchezo wa pete hatua ya nusu fainali, katika bonanza hilo.
Wacheza drafti John Gwile (kushoto) na Mohamed Abdallah wakichuana kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News leo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtevu akimpatia cheti cha shukrani Mratibu wa Dar Live, Luqman Maloto kilichotolewa na klabu mwenyeji, Kejo Community.
Mratibu wa Dar Live, Luqman Maloto akionesha cheti cha Heshima kwa Dar Live, kilichotolewa na klabu ya jogging ya Kejo kutoka Temeke.
Msondo Music Band, wakifanya yao jukwaani katika Bonanza la Jogging & Global Breaking News ndani ya Dar Live.
Washiriki kutoka klabu mbalimbali wakiwa tayari kuanza mbio zao kutoka Uwanja wa Taifa kuelekea Ukumbi wa taifa wa Burudani, Dar Live, katika Bonanza la Jogging & Global Breaking News.
Gari la huduma ya kwanza (kushoto) nalo lilikuwepo katika mbio za jogging kwa ajili ya kunusuru wale watakaopata matatizo.
Mkali wa staili ya 'Mapanga' kutoka TMK Halisi, Rashid Ziada 'KR Mulla' akifuatilia kwa karibu shoo ya Msondo ndani ya Dar Live.
(PICHA ZOTE NA NICODEMUS JONAS / GPL)
Next Post Previous Post
Bukobawadau