JAHAZI YATISHA USIKU WA VALENTINE DAR LIVE
Nyomi ya wapendanao ikifuatilia kwa makini burudani.
Zawadi za Valentine zikiuzwa ndani ya Darlive kama zilivyonaswa na kamera yetu.
Mnenguaji wa Jahazi akifanya yake.
Dada huyu alishindwa kujizuia kuyarudi.
Tx Moshi Juniour akimtunza muimbaji wa Jahazi.
Waimbaji wa Jahazi katika picha ya pamoja.
Mzee Yusuph na mkewe Leila wakiongea kitu mbele ya mashabiki.
Mc akiwauliza maswali wapendanao hao.
Mc wa Dar Live, Pamela Daffa akitoa zawadi kwa mashabiki waliopendeza.
... Pamela akitoa zawadi kwa shabiki mwingine aliyependeza.
Leila Yusuf naye alipata zawadi baada ya kupendeza.
Jahazi yatisha Dar Live
Jana wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walifurika kwa wingi ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ambako Bendi ya Taarab ya Jahazi ilitoa burudani ya nguvu.
Ukumbi wa Dar Live ulifurika kiasi cha kufanya hata sehemu ya kutemea mate ikosekane, aidha mashabiki mbalimbali walipata nafasi ya kupiga picha katika Red Carpet na wengine waliopendeza walishinda zawadi kibao.
(PICHA : ISSA MNALLY NA CHANDE ABDALLAH/GPL)