Bukobawadau

KISHINDO CHA AJALI YA SEMI BUKOBA WATU WANUSULIKA KIFO LEO FEB 2,2014

Hivi ndivyo watu walivyonusulika kifo baada ya Gari lenye namba AJB 7188 aina ya Semi, kuferi breki katika eneo lenye barabara kadhaa zinazounganisha kuingia na kutoka mjini Bukoba
 Ajali hii imetokea majira ya saa 11 alasiri  eneo la Rwamishenye (round about)umbali wa km 2 kuingia Mjini Bukoba ambapo lori 'semi trela' limeanguka baada ya kuferi breki .
Hivi ndivyo Gari hilo lilivyo bonyea sehemu ya mbele .
Maelezo  ya awali yanaonyesha mmiliki wa  wa Gari hili ni Mzambia
Eneo hili la Rwamishenye( round about) limeendelea kuwa na Idadi kubwa ya ajali.
Gari lililopata ajali lilikuwa likitokea nchini Afrika ya kusini , kupitia barabara ya Muleba.
Mmoja wa Askari wa usalama barabara akiwa katika eneo la tukio
Kwa wale Wadau wanaochukia nembo na kupenda picha katika hili tunaomba tusameheane !!
 Gari likiwa limealibika baada ya kuferi breki.
 Nambari za Gari lenyewe.
 Muonekano wa Engine baada ya Gari kupata ajali
 Mashuhuda.


Bango linalo onyesha njia panda kuelekea Kyaka Mutukula
 Kuelekea Round about ya kuingia Bukoba Mjini na kuelekea Kyaka Mutukula
 Mashuhuda wa tukio wakiendelea kujiuliza maswali mengi.
Barabara kuu ya  kuelekea Muleba ,
 Hili ndilo Gari lililokuwa mbele ,likiwa limegongwa kwa nyuma  na lile lililopata ajali
Shuhuda wa kwanza wa tukio hili ambaye ndiye Dreva wa Gari aina Seme pichani hapo juu lenye nambari AAM 1165 T ameileza Bukobawadau Blog  kuwa Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Mwenzake ,aliliona lori  hilo likimfuata kwa kasi huku likiwa limepoteza mwelekeo ndipo akajaribu kuegesha pembeni,ambapo liligonga Gari lake kwa nyuma na kufanyikiwa kupungua kasi kidogo,na wenzake wakapata fursa ya kujiokoa kwa kuruka nje.
 Shuhuda anasema; Gari hilo likiendelea kwa mwendo wa kasi  mpaka bondeni kama inavyo onyesha katika pichani, na kama unavyo ona katika video kwa juu ya habari hii.
 Gari la mtoa maelezo likiwa limeegesha pembeni ya barabara.
Magari yote yalikuwa yamepakiza shehena ya Makaa ya Mawe .
 Gari limeferi Breki kuanzia eneo hili maarufu kama 'Amjuju' tayari Gari lilikuwa lisha feri breki, 
Wakazi wa Mji wa Bukoba wakiwa katika eneo la tukio
 Mashuhuda kwa mbali.
 Ajali hii ingeweza kuleta madhara  makubwa na usumbufu kwa wananchi  waliopo maeneo haya
BUKOBAWADAU BLOG tunatumia fursa hii  kutoa angalizo kwa kwa wakazi wa maeneo haya na mipango mji ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara.

Next Post Previous Post
Bukobawadau