KONGAMANO LA WANAWAKE WA KIISLAMU WILAYANI NGARA
Wanawake wa kiislamu wametakiwa kutambua
umuhimu wao katika dini ikiwa ni pamoja na kulinda maadili kwa kuzingatia
mafundisho ya Mwenyezimungu na mtume Mohamadi SAW
Wito huo
ilitolewa juzi na kiongozi wa waislamu wilayani Ngara mkoani Kagera Shekhe
Rajabu Abdallah Msabaha wakati akifungua kongamano la wanawake wa kiislamu linalofanyika kwa siku tatu katika mtaa wa Benaco ulioko
wilayani Ngara
Shekhe Msabaha alisema kuwa wanawake wanao wajibu wa kujifunza dini yao
kwa kuhakikisha wanafuata na kuzingatia maadili mema ili kuweza kurithisha
vizazi vinavyotoka katika migongo na matumbo yao
Alisema
malezi na maadili mema katika familia yanategemea wanawake kwani ndio walimu wa
kwanza kuwafunza watoto katika kufuata misingi inayokubalika katika jamii
waliyomo na dini yao
“Kwa
asilimia kubwa akina mama ni walezi wa
watoto tunao wazaa hivyo mkipata elimu ya dini kwa hakika
mtaisambaza kwa familia na watoto kuwa
na maadili ya kiislamu kisha kupatikana
nusura kutoka kwa Allah S.W”. Alisema Sheikh Rajabu
Kwa upande
wake Imamu Athumani Abubakari Ally
kutoka Msikiti wa istikama ulioko
Ngara mjini aliwahimiza wanawake hao
kufanya ibada za dini yao bila kujivunia ibada zinazofanywa na waume ama watoto walioko katika familia.
Alisema
kuwa wanawake wanatakiwa kupata elimu ya
kufanya ibada katika taratibu na misingi ya dini hasa kujua namna ya
kusali sala mbalimbali na masharti yake ili kuepuka kufuata matendo bila
elimu inayotakiwa
“Mafundisho
ya Q’urani ambayo ni kitabu cha Allah na hadithi za Mtume SAW ni kuhakikisha
wanawake na wanaume wanakuwa na maadili kwa misingi ya imani ya dini
pamoja na kuvaa mavazi ya kusitiri miili kiislamu”.Alisema Athuman Ally
Aidha
mwenyekiti wa wanawake wa kiislamu
wilayani Ngara Bi Zaria Mohamudu alisema malengo ya kongamano hilo ni kuwafunza wanawake kuzijua
haki zao kidini na kwenye jamii na kuondoa vitendo vya kunyanyasika
kwenye familia
Alisema kuwa
jambo lingine ni kuhakikisha wanapata elimu ya ujasiliamali na kujikwamua
kiuchumi kwa kutumia misingi inayokubaliwa na dini ya kiislamu kwa kuepuka kutoa na kuchukua mikopo yenye riba.
Kongamano
hilo lilihudhuriwa na wahadhiri wa kiislamu kutoka wilayani Ngara na wilaya nyingine
mkoani Kagera pamoja na waliotokea
Mwanza na Nairobi kwa kutoa mada za ndoa taraka na mirathi kwa wanawake na haki
zao katika familia.Na Shaaban Nassibu Ndyamukama