Bukobawadau

BARAZA LA WAZEE WA YANGA LASITISHA MAANDAMANO

Baraza la wazee wa Klabu ya Yanga, leo limetoa tamko la kusitisha maandamano yao ambayo walikuwa wameyapanga kufanyika ili kushinikiza serikali kutoa kibali cha Ujenzi wa uwanja wao wa kisasa unaotarajia kujengwa sehemu ya Jangwani, Dar es Salaam.
Tamko hilo la kusitisha maandamano hayo limetoleo mara baada ya baadhi ya viongozi wa juu wa timu hiyo kukutana na viongozi wa serikali.
Viongozi hao wa serikali walitoa tamko kuhusu kushughulikia ombi lao hali iliyosababisha viongozi wa Yanga kusitisha maandamano yao waliyokuwa wameyapanga kuyafanya juma hili.
Juma lililopita Katibu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali alitoa siku tano kwa Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala, liwe limewapa kibali cha ujenzi huo, vinginevyo waliahidi kufanya maandamano makubwa.
Amesema  viongozi wa juu wa klabu hiyo walikutana na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik, Meya wa Ilala Jery Silaa na Diwani wa Kata ya Jangwani ambapo walikubaliana ombi lao kufanyiwa kazi.
Akilimali amesema serikali kupitia Manispaa ya Ilala ilieleza kuwa ombi lao linashughulikiwa kwa haraka, hivyo aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuelewa jambo hilo bila kuwepo na migogoro.
Ameweka wazi kuwa wanaamini serikali kupitia Manspaa ya Ilala watalishughulikia ombi lao, ingawa amesisitiza kuwa ikitokea ombi lao hilo linaloshughulikiwa likija na majibu ya “hapana” watatafuta mbinu nyingine.
"Sisi tumeomba hivyo majibu ni mawili ndiyo tumepata au tumekosa, ikitokea likaja jibu la kukosa hapo ndiyo kutakuwa na utata na kuamua cha kufanya," alisema katibu huyo wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga.
Ameongezea kuwa klabu hiyo imejiandaa kuwalipa watu waliongezeka katika eneo lao, hivyo hawaoni sababu za kwenda kujenga nje ya mji wakati wao ni watoto wa mjini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau