Bukobawadau

CAMERA YETU MJINI BUKOBA MARCHI 11,2014

Hii ni taswira  sehemu ya mji wa Bukoba kwa juu, haya ni maeneo ya Uswahilini Bilele,ulipo Msikiti wa Jamia na Uwanja wa Uhuru.
Muonekano wa majengo mbalimbali,Uwanja wa ndege na kanisa kuu katoliki Jimbo la Bukoba
Wanamama katika maandalizi ya msosi katika  moja ya shughuli nje ya Mji wa Bukoba
Camera yetu ikiendelea kuangaza huku na kule inakutana na zogo la wananchi likiendelea.
 Mzozo huu unahusu Dada mtu aliyetokea Wilayani Karagwe aliyefika Mjini hapa kumtafuta Kaka yake,mara  baada ya Mwanadada huyo kumpata Kaka yake waliweza  kuongea na kukubaliana juu ya kusudio la ujio
  Kwa heshima Mwanadada alimtaka Kaka yake Mwenye Rasta Kichwani, kunyoa rasta hizo ,baada wakaongozana mpaka Mitaa ya Nkango Miembeni kwa Mzee Baruti ilipo moja ya Saloon ya Kiume ya kisasa,Baada ya kuingia ndani ya saloon na kukakaa kwenye viti,wakati kinyozi anajiandaa ghafla mchezo ukabadilika,Rastaman akajifanya  aelewi somo ,ikatokea mtafaruku mkubwa mtu na dada yake wakazipiga  kavu kavu.Rasta akazidiwa na  kuchomoka mbio.
Mshikaji mbio mbaya akisema ; kuliko ninyoe rasta zangu bora nife!!
Anaonekana Dada mtu mbele ya Mashuhuda wa tukio hili akielezea namna Kaka yake mwenye Imani ya  RASTAFARIAN alivyo mtata ,kitu kinacho wapa Presha wazazi wetu  huko Kijijini ,Rasta apendi Kazi hutumia muda wake mwingi kusikiliza burudani na Uvutaji wa Bangi.
 Dada mtu akitoa Maelezo mbele ya Camera ya Bukobawadau Blog.
 Mshikaji aka Madrid Yuleee anavaa kofia yake  unaambiwa anapenda Rasta zaidi ya Binti anavyopenda Kanga!!!



Next Post Previous Post
Bukobawadau