Bukobawadau

HUKO TABORA WATOTO WATEKETEA KWA MOTO

Watoto waliokuwa wamelala na kuteketea kwa moto ambapo chanzo chake inasemekana ni hitilafu ya umeme.
Miili ya watoto wawili wa familia moja Daniel Paul(8) na Mdogo wake Emmanuel Paul(3)ambao wamepoteza maisha baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani peke yao majira ya saa moja asubuhi,tukio hilo limetokea eneo la Rufita Mwanza road ndani ya Mji wa Tabora.
Katikati ni Ndg Paul Daniel (aliyeshika kichwa) ndiye baba wa watoto waliopoteza maisha kwa moto,haikufaha mika mara moja baba huyo alikuwa wapi wakati tukio hili linatokea.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Bwana Suleiman Kumchaya alifika eneo la tukio mapema wakati kikosi cha zimamoto kikimalizia zoezi la uzimaji wa moto na kutoa miili ya watoto hao ikiwa tayari mauti yamewafika.
 Mwanamama pichani na mtoto ni mmoja wa waliosalimika katika tukio hilo la moto kwa kile kinacho aminika kuwa walikuwa kwenye vyumba vingine.
Baadhi ya samani zilizoteketea vibaya kwa moto.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora OCD Samwel Mwampashe akizungumza na wananchi katika eneo la tukio la kusikitisha lililotekea na kupoteza maisha ya watoto hao.
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau