KAMATI ZA TROIKA ZA MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI, PACIFIC NA JUMUIYA YA ULAYA ZAKUTANA
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi
wa Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala (
mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja
na Wajumbe wa kamati za Troika za Mabalozi wa ACP na Jumuiya ya
Ulaya. Kamati hizo zimekutana leo Brussels kuweka mikakati ya pamoja ya
kuimarisha ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya. Kulia kwa Balozi
Kamala, ni Balozi Mhe. Dimitrious Touloupas Mwenyekiti wa Mabalozi wa
Jumuiya ya Ulaya na Mwakilishi wa Ugiriki katika Kamati ya Siasa na
Usalama ya Jumuiya ya Ulaya.