MAANDALIZI YA YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA MEI 2, 2014 MKOANI KAGERA
Mkoa wa Kagera uanendelea na
Maandalizi ya uzinduzi wa Mbioa za Mwenge wa Uhuru Kitaifa utakaozinduliwa Kaitaba Manispaa ya Bukoba tarehe 02/05/2014
kuanzaia saa moja asubuhi.
Katika maandalizi hayo shughuli
mbalimbali za maandalizi zinaendelea mkoani hapa ambapo maandalizi ya uwanja wa
kaitaba kuwekwa sawa yanaendelea, ujenzi na ukarabati wa mambo mbalimbali
unaendelea kufanyika katika uwanja huo.
Kamati ya sherehe ya mkoa chini
ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe inaendelea na vikao vyake vya kufanikisha uzinduzi huo ambapo kikao kimefanyika trehe 27/03/2014 aidha, kikao kingingine kinatarajiwa kufanyika 15 April, 2014
Pamoja na vikao hivyo kamati
ndogo mbalimbali za shughuli hiyo ya uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru zinaendelea na
majukumu yake kuhakikisha siku hiyo shughuli zinafanyika kama ilivyopangwa kwa kiwango
na ufanisi mkubwa.
Pamoja na shughuli hizo pia
maandaliza ya halaiki yanaendelea kwa walimu na wakufunzi kuendelea na mafunzo
kwa watoto watakaoifanya siku hiyo kufana
kwa ustadi mkubwa ambao wataupata kutoka kwa wataalam wa shughuli za
halaiki.
Wananchi wa Mkoa wa Kagera na nje
ya mkoa wa Kagera mnaalikwa kufika siku hiyo ya uzinduzi wa Mbio za mwenge wa
uhuru hapa mkoani Kagera katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba ili
kujionea tukio hilo la kihistori na kumbukumbu kwa mkoa wetu na taifa kwa
ujumla.
Tukio hilo si la kukosa kwani Mwenge wa Uhuru huleta nuru penye giza,
huleta amani penye mfarakano,Mwenge wa Uhuru pia hueneza huleta upendo na
mshikamao ndani ya wananchi kwa kuwaunganisha na kuwaleta pamoja.
Wanakagera tudumishe mshikamano
na upendo na ukarimukwa kipindi chote ambacho tunatarajia kupokea wageni
mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha wanafika mkoani kwetu
kuhudhuria uzinduzi na kuondoka kwa amani.
Pia kama ilivyo kawaida yetu
Wanakagera kuuweka mkoa wetu safi kila
mara tunakumbushwa kuendelea na utaratibu huo na kuhakikisha kuwa maeneo yetu
yanakuwa safi nay a kuvutia kama ilivyo siku zote ili kuufanya uzinduzi wa mbio
za Mwenge Kitaifa mwaka huu kung’ara
zaidi.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014