MTANGAZAJI WA CHANNEL TEN SALUM MKAMBALA APATA AJALI
Mtangazaji
wa Channel Ten, Salum Mkambala (pichani) amepata ajali ya gari ambalo
alikuwa akiendesha kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro. Kwa mujibu
wa mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten ambaye ameidokeza Global
Publishers.info, Mkambala alipata ajali hiyo maeneo ya Chalinze alfajiri
ya leo na hali yake inaelezwa kuwa ni mahututi baada ya kuumia vibaya.
Haijafahamika yuko hospitali gani kwani alikuwa peke yake kwenye gari
na taarifa ilitolewa na msamaria mwema kwa simu ya Salum na baada ya
hapo simu yake haipatikana tena.
source:GPL