Bukobawadau

MTAZAMO WETU LEO JUMATATU MARCHI 10,1014

BUNGE LA KATIBA
Tusipoangalia kuna hali ya hatari huko mbeleni kwa baadhi ya watu na Taifa kwa ujumla! Ucheleweshaji wa bunge la katiba kumaliza muda wake mapema, kutapelekea bunge la bajeti kuchelewa!! Ucheleweshaji wa bunge la bajeti utapelekea ucheleweshaji wa kuanza kwa financial year(In real terms) japo kimaandishi mwaka wa fedha unaanza Julai(In nominal terms).
Kuchelewa kwa mwaka wa fedha inamaanisha serikali haitaweza kutoa pesa mapema (allocations and release of funds). Uhaba wa pesa, utapelekea shughuli nyingi za kiuchumi na maendeleo kwa ujumla kukwama! Wanaofanya biashara na serikali hawatalipwa kwa wakati, idara nyingi za serikali, Taasisi na kwenye halmashauri zetu, mambo yatasimama! Kwa sababu wafanyabiashara wengi wanategemea government money, ukopaji katiba mabenki utadorola na benki zitashindwa kufanya biashara!

NI MTAZAMO WETU, ILA WACHUMI WANAWEZA KUTUSAIDIA KATIKA HILI!!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau