Bukobawadau

MTOTO QIAN ALIYE USHANGAZA ULIMWENGU MWAKA 2012

Mwaka 2000, mtoto Qian Hongyan, aliumia katika ajali mbaya ya gari akiwa na umri wa miaka mitatu. Ili kuweza kuishi madaktari bingwa iliwalazimu wamkate miguu yake miwili na kumwekea mpira uliomfanya aweze kuutumia kama miguu.

Wazazi wa Qian, wanaishi katika mji wa Zhuangxia nchini china na hawakuwa na uwezo wa kumpatia vifaa vya kisasa ili aweze kuvitumia katika mwili wake badala yake akawa anatumia nusu ya mpira wa kikapu (basketbal) ukanyagia ardhini.

Akatumia na vibao viwili mkononi pamoja na mpira ule ili aweze kutembea. Mtoto Qian alijitahidi kutumia mpira ule ili aweze kuishi, kwenda shuleni pamoja na kucheza kama msaada wake.

Qian Hongyan ambaye alilazamika kutumia vifaa vile aliushangaza ulimwengu na mamilioni ya watu wake na ndoto yake ya kwenda kushindana katika mashindano ya kuogelea yaliyofanyika mwaka 2012 mjini London uingereza.
Hadithi ya mtoto Qian ikasambaa na kuifikia serikali ya china kupitia kitengo maalumu cha utafiti wa watu wenye ulemavu katika jamii na hatimaye wakamsaidia na kumpa vifaa vya kisasa ili aachane kutuumia ule mpira

Qian sasa anayo miguu ya bandia aliyotengenezewa lakini yeye bado anadai kuwa anapenda sana kuutumia ule mpira kwani una mpa urahisi kuingia na kutoka katika mabwawa ya kuogelea kila mara aogeleapo.

Mungu ambariki mtoto huyu ambaye aliushangaza ulimwengu kwa kuonyesha ujasiri wake

FUNZO

Kila mara jaribu kuhesabu baraka ulizojaliwa katika maisha yako na kama utaona matatizo yamezidi kuliko baraka basi rudia kuhesabu upya.

kwa kuwa twatumia muda mwingi kujilaumu kwa matatizo yatupatayo na kusahau kuwa kuna baraka tumezikalia na hatuzitambui.

Mungu yu mwema nyakati zote
Comment ASANTE na kisha share kumshukuru Mungu kwa baraka alizokujalia katika maisha yako

BUKOBAWADAU BLOG Tunakutakia Jumapili Njema na Kwaresma Njema
Next Post Previous Post
Bukobawadau