Bukobawadau

MTOTO WA WAZIRI AZUIA NDEGE KUTUA


Shirika la ndege la MEA lasema ndege yake iliyokuwa na abiria 71 ililazimika kurudi Beirut baada ya mtoto wa kiume wa waziri wa uchukuzi wa Iraq kuchelewa kuabiri na kupiga simu Baghdad akiomba ndege hiyo izuiwe kutua.
Ndege ya shirika la ndege la Mashariki ya Kati (MEA) iliyokuwa ikitoka Lebanon kuelekea Iraq ililazimika kurejea ilikotoka ikiwa katikati ya safari Alhamis, baada ya mtoto wa kiume wa waziri wa uchukuzi wa Iraq kuchelewa kuabiri ndege hiyo kwa wakati na kupiga simu Baghdad akiomba ndege hiyo izuiwe kutua.
Shirika hilo la ndege linasema ndege yake ililazimika kurudi nyuma baada ya kuwa angani kwa dakika 21.Ndege hiyo ya shirika la MEA ilichelewa kuondoka kwa dakika sita kwa sababu ya kumkosa abiria mmoja aliyetambulishwa na shirika hilo lenye makao yake Beirut, kama mwana wa kiume wa waziri wa uchukuzi wa Iraq Hadi al-Ameri.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 71 ilikataliwa kutua Baghdad na kurejea Beirut. Huko Baghdad, msemaji wa waziri mkuu Nouri al-Maliki alisema Bw. Maliki ameamrisha waliofanya maamuzi hayo wafutwe kazi.
Chanzo, voaswahili
Next Post Previous Post
Bukobawadau