Bukobawadau

MUHIMU KATIKA MAHUSIANO

Hatakama mazingira ya mahusiano yako yanaonyesha chuki, bado ni uchaguzi wako kuamua kumchukia au kumpenda mpenzi wako. Sio marazote kwenye mahusiano tunapenda tunapopendwa na kuchukia tunapochukiwa, maranyingine tunapokuwa tumemaanisha katika mahusiano yetu tunalazimika kuonyesha upendo hata pale tusipoheshimika au kuheshimu hata pale upendo unapopungua. Najua ni ngumu lakini inawezekana, “it is hard but it is worthy it”
 KATIKA MAHUSIANO
Katika mahusiano yako ni vema ukafahamu kwamba kila kitu unachokifanya au kukisema, kiwe kibaya au kizuri kina matokeo au athari katika mahusiano yenu, hatakama wakati kitu hicho kinafanywa au kinasemwa mpenzi wako hakugundua au kukitilia maanani. Usiendekeze sana maisha ya siri hata kama wewe ni mzuri sana wa mikakati ya kujitetea “excuses” ipo siku utakosa pakupenyea na kwa bahati mbaya unaweza kumkosa uliyempenda. Remember “what goes around comes around”
Next Post Previous Post
Bukobawadau