Bukobawadau

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AMENASWA LAIVU AKIJIUZA

Pichani Mwalimu akiwa ameduwaa baada ya kunaswa kwenye sakata hilo.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar.Machi 24, mwaka huu ambapo awali, wakazi wa eneo hilo waliwatonya mapaparazi wa Operesheni Fichua Maovu (OFM) kuwa kuna danguro kubwa maeneo ya Kizuiani ambalo limesheheni madadapoa wa kila aina wakiwemo mabinti wadogo.
Chanzo hicho kilimwaga data kuwa, kuna mzee maarufu kwa jina la babu katika eneo hilo ambaye amekuwa akiwapa machangudoa hifadhi katika banda lake na kuwapa magodoro chakavu kwa malipo ya shilingi elfu moja kwa kila kichwa.
KISIKIE CHANZO
“Jamani kwenye danguro hili kila aina ya uchafu upo. Wanatukwaza sisi Wakristo ambao tupo katika kipindi hiki cha Kwaresma,” kilitiririka chanzo hicho cha kuaminika maeneo hayo.
OFM KAZINI
Ili kujiridhisha na taarifa hizo, makamanda wawili wa OFM walitimba katika danguro hilo wakajifanya wateja ambapo walimchukua mmoja na kubaini kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau