SERIKALI YA MALAYSIA YADHIBITISHA KUWA NDEGE ILIANGUKA KUSINI MWA BAHARI YA HINDI NA ABIRIA WOTE 239 HAKUNA ALIYEPONA
Huu ni ujumbe rasmi toka mamlaka za Malaysia, kwenda kwa ndugu, jamaa na
marafiki wa waliokuwa abiria 239, wa ndege MH370, ya shirika la ndege la
Malaysia, iliyopotea zaidi ya wiki mbili sasa. Mbali ya kujulishwa kwa
njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (SMS), pia Waziri
Mkuu wa Malaysia, Najib Razak, amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na
kutoa ujumbe huu live.