Bukobawadau

BAADA YA NGARA KUTANGAZA UFAULU WA BRN, BIHARAMULO WASHINDI KIMKOA WATAKA UFAULU KITAIFA

Kaimu Afisa elimu wilayani Biharamulo Samwel Sammy akipanda mti katika shule ya msingi Nyamigogo iliyokuwa ya kwanza kiwilaya na kikata ikiwa ya 10 kimkoa na 26 kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Biharamulo na diwani wa kata ya Nyakahura Apolinary Mugarula
Katibu wa ccm wilayani Biharamulo Odilia Maholelo
 Mratibu elimu Kata ya Nyamigogo Ailigi Manyesi akishiriki kupanda mti katika shule ya msingi Nyamigogo iliyokuwa ya kwanza kiwilaya na kikata ikiwa ya 10 kimkoa na 26 kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana
 Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamigogo wilayani Biharamulo Mkoani Kagera wakiwa kwenye burudani ya kusherehekea ushindi wa kitaaluma wilayani humo jana kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu shuleni hapo
 Burudani ikiendelea
 Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamigogo wilayani Biharamulo wakiendelea na burudani
 WILAYA ya Biharamulo Mkoani Kagera ambayo katika matokeo ya ufaulu wa mitihani ya elimu ya msingi mwaka jana ilikuwa ya kwanza kimkoa na ya pili kitaifa imejipanga tena kuwa ya kwanza kwa matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka mwaka huu

Kaimu Afisa Elimu wilayani Biharamulo Samweli Sammy amesema hayo jana (April 9) katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika katika shule ya msingi Nyamigogo iliyokuwa shule ya kwanza wilayani humo kwa matokeo ya  mwaka jana
 Sammy alisema ufaulu huo utazingatiwa kwa kusimamia taaluma katika shule zote zipatazo 88 zenye wanafunzi 50711 kati yao wavulana  ni 24 966 na wasichana ni      25 745 wanaofundishwa na walimu 858 waliopo kati ya 1287 wanaohitajika.

Alisema  mikakati iliyopo katika idara hiyo ni kufanya majaribio ya mitihani ya usuli (Mock) kwa wanafunzi wa darasa la saba na la nne  ili kuwafanya wanafunzi kujenga uzoefu wa kujibu maswali ya mitihani.


“Mafanikio yatapatikana kwa kutekeleza ugatuaji madaraka kwa walimu na kuwa na utawala bora kisha  kutekeleza mapendekezo ya wakaguzi ikiwa ni pamoja na kutatua kero za walimu kadri ya uwezo utakavyoruhusu”.Alisema


Aidha aliongeza kuwa mikakati mingine ni kufanya tafiti za kielimu kubaini kero ili kuzifanyia ufumbuzi kwa kulenga kufanikisha  mpango wa kitaifa wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now)

 Pamoja na malengo hayo zilitajwa  baadhi ya changamoto kuwa ni upungufu wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia hasa vyumba vya madarasa 798 ili  kukidhi mahitaji ya vyumba  1415 kupunguza msongamano wa wanafuzi katika darasa moja.

Upungufu mwingine ni nyumba 962 za walimu kwani  walimu wanne hukaa katika nyumba moja huku  wanafuzi wakihitaji kuongezewa matundu ya vyoo 873 na  yaliyopo ni 1085 kwa wastani wanafunzi 47 hutumia tundu  moja badala ya wafafuzi 25.

 Hata hivyo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Biharamulo Richard Mbeho  aliwashauri viongozi wa idara ya elimu na kata ya Nyamigogo wilayani humo kutobweteka na ufaulu walioupata mwaka jana kuepuka kurudi nyuma kitaaluma

Alisema uongozi wa elimu kwa kushirikiana  na ofisi za mipango katika halmashauri ya wilaya hiyo baadhi ya changamoto zinaweza kutafutiwa ufumbuzi kama kutakuwepo ushirikishaji wa jamii hasa ukusanyaji wa vifaa vinavyopatikana kwa wananchi.

Viongozi mbalimbali wilayani Biharamulo waliohudhuria kilele cha wiki ya elimu katika shule na kata ya Nyamigogo walifanya zoezi la upandaji miti katika shule ya Nyamigogo

   Na Shaaban Ndyamukama April 11, 2014                                                   
Next Post Previous Post
Bukobawadau