Bukobawadau

BALAA!! AJALI NYINGINE YATOKEA BK RWAMISHENYE (ROUND ABAUT) ASUBUHI YA LEO APRILI 12, 2014

Taswira hii ndivyo ilivyo hali ya hewa kwa kutwa ya leo Jummosi Aprili 12,2014 ,Kupitia Bukobawadau Blog.
 Hivi ndivyo Gari lilivyogonga hodi sebuleni kwa mtu asubuhi ya leo majira ya Saa tatu na nusu,Tukio hili ni baada Gari aina ya fuso likiwa limepakia mchanga kuferi breki katika eneo lenye barabara kadhaa zinazounganisha kuingia na kutoka ndani ya Manispa ya mji wa Bukoba
 Eneo la round about ya Rwamishenye Bukoba.
Tukio hili ambalo limetisha kwa mguso na athari yake katika jamii , lingeweza kuleta madhara  makubwa na usumbufu kwa wananchi  waliopo maeneo haya, angalizo 'Kama jamii tunaendeleza na kujenga mfumo wa fikra na mawazo  ya kwamba ni mara chache mgari kuferi breki na kushindwa kukata kona basi tutegemee Makubwa zaidi ya hili'.
Muonekano wa Gari likiwa limegonga hodi Sebuleni kwa mtu na kuvunja madirisha, ni tukio la nne katika mfululizo wa ajali katika eneo hili la Rwamishenye (round about) ,hoja ni mikakati gani inayofanywa na viongozi katika ngazi mbalimbali za kijamii na kiserikali kubuni na kujaribisha mikakati kwa ajili ya kunusuru wakazi wa maeneo haya?!!
Nyumba hii hii ni mali ya familia maarufu ya 'Mnyinge'
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio
 Alama za matairi ya gari zilizoelekea kwenye eneo la tukio


Sehemu iliyo gongwa na Gari hili wakati linaachia  njia.
 Mti uliogongwa baada ya gari hilo kuachia njia, ukiwa umeanguka
Gali likiwa tayari limegonga ukuta wa Nyumba.
 Taswira ya tukio kamili
 Wanadada pichani wamenusurika fifo kutokana na gari hilo kugongwa chumba cha sebule Jirani yao
Makutano yae barabara kadhaa zinazounganisha kuingia na kutoka Mjini hapa.
 Abajulizi!
Kwa mara nyingi BUKOBAWADAU BLOG tunatumia fursa hii  kutoa angalizo kwa  wakazi wa maeneo haya na viongozi katika ngazi mbalimbali za kijamii na kiserikali kubuni mikakati ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara.
Next Post Previous Post
Bukobawadau