Bukobawadau

HALI NI MBAYA KWA WANA KAGERA,SALAM KUTOKA KWA MDAU!

Nimekuwa nikitembelea vijiji mbalimbali Tanzania, ukienda huko vijijini unaweza ukajiuliza hivi hawa watu wanaishi vipi?.
Ukitazama mashamba yao ni kilimo cha mikono, wanalima kwa kutumia mvua, hawajui kama watavuna au laa, mwaka huu al hamdrullah wamepata mvua, hali ya ukame kwa miaka ya karibuni imekithiri.
Sehemu zingine Tanzania angalau wana ardhi ya kutosha kulima na kufuga, akiuza debe la mahindi na mbuzi siku zinasonga mbele.

 Kwa upande wa Kagera hali inasikitisha, kuna ugonjwa uliovamia migomba unaitwa mnyauko, huko mashamba ni madogo, kahawa bei imekufa. Lakini hata kama kahawa ingekuwa na soko mashamba ni madogo. Nilikuwa huko, nikawa najiuliza hivi hawa wananchi wanauza nini ili waishi, ukienda huko watu bado wanakopeshana shilingi mia mbili.
Utafiti wangu kwa ujumla unaonesha vijijini watu wanaishi kwa kula mlo mmoja, wa tena mboga za majani kila siku kwa kuwa zinapatikana maporini kirahisi.

 HALI ya mkoa wa kagera inaenda kwenye crisis,stendi ya mabasi ya mkoa ni kama zizi la mbuzi,usiende na kiatu cheusi,,*matope yanatisha,soko la pale mjini ni janga,ni kama msiba unaendelea pale na limechakaa,bukoba wamegoma kupimiwa viwanja,the whole town is marked by squatter,kama walivyosema hapo juu,uchumi unadorora kwa kasi kubwa,uzalishaji ndizi uko chini kuliko wakati wowote,pia kahawa,POPULATION YA KAGERA ni tishio kwa uchumi hasa mgawanyo wa ardhi per person.
MWISHO:HALI HIYO IMECHOCHEA MAJUNGU KATI YA WANASIASA,NA KATI YAWATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI,OLE WAKO UPANGIWE KAZI YA KISERIKALI KAGERA!!! 
SALAM KUTOKA KWA WADAU VIA JF
Next Post Previous Post
Bukobawadau