KIJIJI CHA BUGORORA MISSENYI NA HARAKATI ZA MAENDELEO
Ndugu Frederick Kamugisha pichani, Mweyekiti wa Tujunangane Saccas Bugorora.
Wananchi hawako nyuma katika kushiriki maamuzi,huu nni mkutano wa halmashauri ya kijiji ambao Afisa mtendaji wa kata ya Bugorora Bi Anastella Gabriel(mbele mwenye ushungi)alialikwa.
Vijana wa kijiji hicho hawako nyuma katika shughuli za uzalishaji mali.Huu ni mradi wa marando kwa ajili ya kuzalisha na kuuza ili jamii izalishe viazi lishe vinavyotumiwa na akina mama wajawazito na watoto,na pia kutengenezea vitafunwa kama maandazi n.k(kwenye kitalu marando huhifadhiwa kwenye wavu kwa ajili ya usalama)
Kaimu Afisa mtendaji wa kijiji cha Bugorora,Bi Anastazia Thobias akichangia kwenye mkutano wa halmashauri ya kijiji,aliye kaa pichani kushoto ni mwenyekiti wa muda wa kijiji hicho Ndugu Frederick Fransis
NA MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi
KIJIJI cha Bugorora katika kata ya Bugorora ni miongoni mwa vijiji vya kupigiwa mfano wilayani Missenyi katika harakati za wananchi wake kujiletea maendeleo.
Mwandishi wa habari wa Bukobawadau aliyekuwa kijijini humo mwishoni mwa juma alikutana na mwekahazina wa kikundi cha kusaidiana kinachoitwa Tujunangane Saccas Bugorora,Frederick Kamugisha.
Anasema kikundi chao kilianzishwa 5 Julai 2013 kikiwa na wanachama 23, chini ya mradi wa DASIP wa Halmashauri ya wilaya ya Missenyi,na kuwa sasa kina wanachama 45 katika mpango wa kuweka na kukopa.
Anasema kikundi chao kilianzishwa 5 Julai 2013 kikiwa na wanachama 23, chini ya mradi wa DASIP wa Halmashauri ya wilaya ya Missenyi,na kuwa sasa kina wanachama 45 katika mpango wa kuweka na kukopa.
Kamugisha anaeleza kuwa maana ya saccas ni ngazi ya kwanza kabla ya kufuzu kuandikishwa kuwa saccos na kuwa wana mtaji wa zaidi ya sh milioni tatu na laki tatu walizoweka benki kutokana na
kiingilio,hisa,amana na riba na kuwa mtu hukopa mara tatu ya hisa alizoweka.
“Kwa kweli mpango huu umekuwa wa manufaa kwetu.Huko nyuma ukiwa na shida unakwenda kwa mtu,unaeleza matatizo yako yote,anasikiliza siri zako zote,kisha anasema hana hela hata kama anayo.Sasa mambo ni tofauti kabisa”,anasema mwekahazina huyo.

Jambo jingine la kufurahisha kuhusu umoja wao ni kwamba hakuna mwanachama yeyote aliyewahi kupotea na mkopo kama inavyosikika katika sehemu nyingine,na hiyo wanasema ni kutokana na masharti magumu ya kuchukua mkopo,lakini waliyokubaliana ikiwa ni kuweka rehani mali isiyohamishika ambapo wadhamini wanaotakiwa kusaini ni mke/mme na watoto.
Hata hivyo kijiji hicho kinakabiliwa na uharibifu wa mazingira kama uchimbaji mchanga kwenye hifadhi ya barabara ya Bugorora-Kabingo.