MAANDALIZI YA BIRTHDAY PARTY YA BI RUKIA KASSIM KUPAMBWA NA UZINDUZI WA MWENGE MAY 2,2014
Ngoma za masikio ya mwanalibeneka wenu (kiranja)wa Bukobawadau Blog yamenasa fununu za kuwepo kwa pati ya aina yake mwishoni mwa wiki hii itakayo fanyika ndani ya Ukumbi wa Linas Night Club.
Ndipo tukaanza kuandaa ‘patroo’
maalumu ili kunasa habari za hapa na pale kujua ni nini kitakachojili na patakuwa na matukio yapi muhimu.
Chanzo chetu kinabaini
kuwa, maandalizi ya sherehe hiyo tayari yameingiliwa kati kati na Mme
wake Mdau Abdulrahim Mawenya (Mr Simba) na kumzuia BI Rukia asitumie fedha zake na
kwamba kila kitu na gharama zote za juu zitakuwa juu yake.
Akizungumza na waandishi wetu kwa usiri na sauti ya ‘kimbeya’, mmoja wa
rafiki wa (jina (kapuni) aliweka wazi kwamba Mr Simba amepania
kumfanyia Mke wake mpendwa pati hiyo ikiwa ni moja ya matukio yatakayoendelea
kukumbukwa kwa mwaka huu.
“Bwana Abdulrahim Simba amepania kufanya
makubwa kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa ya MKEWE ikiwa ni moja ya
matukio yake muhimu yatakayokumbukwa. Itakuwa ni
pati ya kufa mtu,” alisema
Katika moja ya maandalizi ya sherehe hiyo itakayo fanyika siku ya UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA MJINI HAPA tayari wamealikwa watu maalum ,pia vikundi vya burudani na wacheza show maalum.
Katika sherehe hiyo ambayo Bi Rukia anatimiza miaka kadhaa tangu
aanze kuvuta hewa ya oksijeni, muziki wa ladha mbalimbali utatawala; Bongo, Sebene,Kwaito, RnB, Eningiri, omutoro,okwebuga,Enchuma aka Sindika!!na
nyimbo za wasanii wengineo wa hapa Nyumbani zitasikika masikioni mwa watakao hudhuria.
FANYA UWEZAVYO MDAU ,UWE MMOJA KATI YA WENYE BAHATI YA KUHUDHURIA PARTY HII!!