Bukobawadau

HARUSI KUTOKA MAKTABA YETU,UJANJA NI KUPUNGUZA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA!

Ni mara chache sana kuona ndoa na sherehe za aina hii, wahusika  ni watu wanne tu maharusi na wapambe wao.
 Ni harusi ya Bwana Joseph Mulokozi na Bi  Leoncia  Alimwambaza pichani muda mchache baada ya Ndoa takatifu na kuendelea na sherehe fupi iliofanyika katika Viwanja vya Gymkhana eneo la  Bukoba Club,ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba
Kuna haja gani vikao kumi vya maandalizi mpaka usiku wa manane hadi mkuu wa mkoa kalipigia sana kelele. Vikao vingine watu wanakaa mpaka kuumwa na Mbu.
Michango mpaka mamilioni wakati elfu 20 tu inatosha na kwa Bukoba mjini sasa,ndo hatari kuna  Kapu la mama (mjuburo),siku ya harusi yenyewe Burudani,mc,zawadi ya mama,Mjomba, Bibi,Babu, mshenga, Wanakamati,Vikundi vya kukopeshana vya kinamama hapo sasa wanakuja wanawake 20 wamebeba ndoo moja ya plastik inauzwa elfu 4000.

 Foleni ya Chakula ndefu kama foleni ya Sukari,Kufungua muziki saa 8 Maharusi wapo hoooi(chockest ile mbayaaa)yote ya nini jamani?!!Noma sana!!!
 Taste Africa’s world class beer. Windhoek Lager 100% PURE BEER
Timu nzima ya Bukobawadau  Blog tunawapongeza sana wadau hawa na huu ni mfano bora.!!


Next Post Previous Post
Bukobawadau