Bukobawadau

MWANAFUNZI AUAWA NA KUNYOFOLEWA VIUNGO VYA MWILI

MULEBA:Na Shaaban Ndyamukama May 2014

Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kitunga wilayani Muleba mkoani Kagera ameuawa na mganga wa kienyeji kwa kunyonga kisha kumzika nyumbani kwake kwa kile kilichodaiwa ni imani za ushirikina

Afisa mtendaji wa kata  Muhutwe wilayani Muleba Wilson Charles amesema mwanafunzi huyo wa kike (8) jina limehifadhiwa (Furaha Jofule) aliuawa juzi  katika kijiji cha Bisole kwa kukatwa  viungo vya mwili  kisha kuzikwa kichwa chini miguu juu

Bw Charles amesema kuwa walikuwa wananfunzi wanne wakielekea shuleni na walipofika njiani waliitwa na mganga wa kienyeji Juma Busigwa  ambapo watatu walikataa na kukubali mmoja wao na ndipo alimkamata kisha kunyonga

Amesema katika kufanya kitendo hicho kwanza alimkata sehemu zake za siri masikio sehemu ya mabega na kukata mkono wa kushoto ambapo alichimba chimo katikati ya mafiga na kutunza viungo hivyo vya mwili wa mtoto huyo

“Alipomaliza kuficha viungo ndani ya nyumba alichimba tena shimo kubwa na kumwinamisha kwa kutanguliza kichwa kisha kiuno na miguu kubaki nje yaani alifukia nusu ya kiwiliwili” Alisema Charles

Aidha amesema taarifa za mwanafunzi huyo kuuawa zilipatikana baada ya kutafutwa shuleni bila kupatikana hadi kesho yake ambapo wenake aliokuwa nao ndio walitaja mazingira alipopotelea na alipatikana kwa mganga huyo saa7 mchana

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Bisole  Philbert Ludovick amesema hilo ni tukio la pili katika kijiji hicho kwani mwaka juzi mwanafunzi wa kike alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kupatikana akiwa amechunwa ngozi

Alisema vitendo vya mauaji na kuchukua viungo vya mwili vinafanywa na wageni kutoka nje ya mkoa wa kagera wanaotafuta kupata utajiri wakijiingiza kwenye biashara mbalimbali kwenye maeneo yanayokua kiuchumi na kimaendeleo

“Tuna mji wa Izigo na Kaboya wanakuja watu wengi kuendesha maisha yao lakini licha ya kuwasajili kwenye madaftari ya vitongoji wanaishi kwa kuhama hama na kusabaisha wasitambulike shughuli zao kwa undani”.Alisema Ludovick
Kamanda wa jeshi  la  polisi mkoani Kagera Bw George Mayunga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa ambaye amekiri kufanya mauaji hayo anashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi
Next Post Previous Post
Bukobawadau