Bukobawadau

SIKILIZA KILIO CHA MCHUNGAJI NA 'KONDOO WAKE'

 IMEELEZWA kuwa zaidi ya wanafunzi sabini wa madhehebu mbalimbali ya walokole chini ya mwavuli wa CASFETA katika taasisi moja ya elimu iliyoko kata ya Kanyigo,wilayani hapa hawapati huduma za kiroho kufuatia uongozi wa taasisi hiyo kupiga marufuku huduma hiyo.
Taarifa hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na  mchungaji Douglas Majula wa kanisa la Tanzania Victory Chrisian Centre (TVCC) la Kabambilo kata ya Kanyigo,wakati akihubiri katika ibada ya maziko ya marehemu Judith Amos Kagashe,kijiji cha Bweyunge katani humo.

  Alisema kuwa tangu mwezi Agosti mwaka jana hadi sasa,wanafunzi walokole wa taasisi hiyo ambayo hakuitaja,hawapati somo la dini wala kuhudhuria kanisani siku za Jumapili na hivyo kunyimwa uhuru wa kuabudu tofauti na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayotoa uhuru huo,na kwamba kanisa limewaona viongozi wenye mamlaka katika wilaya na mkoa lakini bado hawajasaidia.
“Kwa haya ninayotamka niko tayari hata kukamatwa,lakini kila ushahidi ninao kwamba hii ni chuki tu dhidi ya wana wa mungu,lakini hatimaye tutashinda”
Hata hivyo imejulikana baadae kuwa wanafunzi hao walizuiliwa ‘kusali’ kutokana na kugomea kushiriki mashindano ya ngoma wakidai ni ngoma za kunengua na ‘kukata mauno’ kinyume na imani yao.

Wanandugu wakiweka maua kaburini
 Mchungaji Douglas Majula akihubiri wakati wa maziko
NA MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi
Next Post Previous Post
Bukobawadau