Bukobawadau

TASWIRA NA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WILAYANI KARAGWE

 Wilaya ya Karagwe inakabiliwa na  changamoto ya upungufu wa watumishi kuanzia ngazi za vijiji hadi wilaya hali inayopelekea kukwamisha shughuli za utoaji huduma kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Karagwe Dary Ibrahimu Rwegasira  katika kikao cha Baraza la madiwani  kilichofanyika  juzi kwenye ukumbi wa  kituo rafiki cha Vijana maarufu kama angaza kilichopo  mjini Kayanga wilayani hapa.
Jengo la Halmashauri ya Wilaya Karagwe.
 Mtaa kwa mtaa Camera yetu inakutana na Rasta mmoja maarufu Wilayani Karagwe
Alisema kuwa wilaya  inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi kuanzia ngazi ya vijiji,kata na wilaya  hali inayosababisha kukwamisha utoaji huduma kwa uhakika na kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.
Rwegasira alisema kuwa  changamoto nyingine zinazoikabili wilaya ya karagwe ni  ugonjwa wa mnyauko wa migomba na ukame ambazo zimeathiri sana maendeleo ya wilaya kwani  wananchi   na wenyeji wa Karagwe hutegemea kilimo cha migomba na mazao mbalimbali ya chakula hivyo ukame umeathiri sana  shughuli za kilimo.
 Aidha,alibainisha kuwa  vitendo vya  unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji  kwa mwaka 2013 vimeongezeka tofauti  na miaka mingine ni kutokana  na kutokuwepo ushirikiano wa wahusika na vyombo vya dola.
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imedhamiria kuwa, katika kipindi cha miaka tisa ijayo, wananchi wa Wilaya hii kwa jinsia zote walioko Wilaya hii wawe jamii yenye maisha bora, inayowajibika kwa maendeleo yake, uchumi imara na endelevu na uongozi unaozingatia mipango shirikishi na utawala wa kisheria ifikapo 2025
Next Post Previous Post
Bukobawadau