Bukobawadau

HATI ZA VIWANJA MANISPAA BUKOBA

Marafiki wapendwa
Pamoja na changamoto, Manispaa ya Bukoba imeandaa hati zaidi ya hati 1,000 kwa walioomba na kulipia viwanja katika mradi wa viwanja 5000.

Orodha hii inajumuisha:
1. Hati ambazo zimeandaliwa, hivyo kuwaomba wahusika kusaini hati hizo. Unaweza ukatuma mwakilisha kukuchukulia ili uweze kusaini na kurejesha ofisi za Manispaa-Idara ya Mipango Miji na Ardhi.
2. Hati ambazo zimekamilika yaani zimeidhinishwa na Kamishina na kusajiliwa na Msajili wa Ardhi Mwanza. Waweza kufika ofisini au kutuma mwakilishi akiwa na Power of Attorney kuchukua hati yako. Hati nyingi zimepelekwa Mwanza ili ziweze kuidhinishwa na kusajiliwa lakini kidogo kutoka kwake ni kudogo sana. Tumewasihi wahusika waweze kuongeza kasi ya kuidhinisha na kusajili.
Wale ambao majina yao hayaonekani na tayari wamekamilisha malipo, tunawaomba wawe na subira, tunaendelea kuandaa. Tutawajulisha kwa simu kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Mjulishe jamaa, rafiki na nduguyo.

RAI: Waliopata viwanja waanze kujenga, shukrani kwa wachache ambao tayari wameanza pia walipe kodi ya ardhi kwa maendeleo ya Manispaa na Taifa kwa ujumla.

Kujua hatua ya maandalizi ya hati  wasiliana na Fauzia Kimaro (0754775309)
Tushabire Bukoba na Kagera
Inawezekana.
Next Post Previous Post
Bukobawadau