Bukobawadau

MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU MZEE REVERIAN MTORE,BUGANGUZI JUNE 27,2014

Shughuli ya Mazishi ya Marehemu Mzee Reverian Mtore, wa Kijijini Katare Buganguzi.
 Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mzee Mtore ikiendelea nyumbani kwake Kijijini Katare, Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba.
Pichani ni Ndugu Ave akiongoza Kundi la waimbaji wa Kwaya ya Mbatama likiungana na wananchi kuimba nyimbo za maombolezo kwa ajili ya Kumuaga Marehemu Mzee Mtore.
 Watu kutoka maeneo mbalimbali wameweza kuhudhuria na kushiriki Mazishi hayo.
 Sehemu ya Waombolezaji wakiendelea na Ibada ya Kumuaga Marehemu Mzee Mtore.
 Misa takatifu ya kumuaga Marehemu Mzee Revelian Mtore Ikiendelea.
 Baada ya Misa, shughuli za mazishi ziliendelea eneo la Makaburi yaliopo Shambani kwa Marehemu.


Mabadre wakiongoza shughuli ya Mazishi.
 Zoezi la kuweka Udongo katika kaburi la Marehemu Mzee Revelian Mtore likiendelea
Utaratibu wa kuweka Udongo Katika Kaburi la Marehemu Mzee Reverian Mtore ukiwa unakamilika.
 Baada ya kuweka udongo kaburini Waombolezaji wakisawazisha Udongo.
Ndugu wa familia na Watoto wa Marehemu wakiwa tayari kuweka Mishumaa na Mashada ya Maua .
Mazishi yakiendelea kwa nyimbo na mapambio ya hapa na pale
  Bi Theonestina Mtore, Mtoto wa Kike wa Marehemu Mzee Mtore akiwa kabeba Msalaba.
 Ndugu Charles Mtore na Mwanae wakiwa tayari kwa ajili ya kuweka Maua kwenye Kaburi
 Mdau Willy Mtabuzi akitoa angalizo flani kwa Padre .
 Tumepokea taarifa kutokandani ya Familia kuwa Shughuli ya Matanga itafanyika siku ya Jumatatu .
 Msalaba ukiwa umeinuliwa juu kabla ya kuwekwa katika Kaburi la Marehemu Mzee Mtore.
Somo la kuweka kando kila mzigo mzito na dhambi.
 Padre akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu Mzee Reverian Mtore.
 Taswira namna watu walivyo shiriki Mazishi hayo, yaliofanyika Jioni ya Leo Ijumaa June 27,2014
Msiba huu ni pigo kwa familia na Wadau waliomfahamu Marehemu Mzee Reverian Mtore.

Katika hali ya Simanzi ya kuondokewa na Baba yake Mzazi anaonekana Mdau Mboma Robart Mtore
 Muonekano wa Kaburi la Marehemu Mzee Mtore.
 Ndugu Charles Mtore, ambaye ndiye mtoto mkubwa wa Marehemu Mzee Mtore akiweka shada la maua kaburini
 Pichani kushoto ni Mzee Elia, Kaka Mkubwa wa Mzee Tibaigana.
Ndugu Charles Kushoto na Mdogo wake John  maarufu kwa jina la Mzee pichani kulia.
 Mzee Shaban pichani katikati na Mzee Lusseta pichani kulia
 Kushoto ni Mdau Avevan Tibaigani.
 Mdau Mzee (John) mmoja kati ya watoto wa Marehemu Mzee Reverian Mtore.
 Mzee Adv.Rweyemamu,Rafiki mkubwa wa Marehemu Mzee Mtore akiweka shada la maua kaburini
 Ndugu Salim Mjukuu wa Marehemu akiwa tayari kuweka shada la Maua Kaburini.
Ni shughuli ya Maziko ya Marehemu Mzee Reverian Mtore.
 Wakwe wa familia ya Marehemu Mzee Mtore kutoka Msoma wakishiriki kutoa heshima zao za mwisho kwa kuweka shada la maua kaburini
Zoezi la kuweka mashada ya Maua Kaburini likiwa linaendelea.
Bi Anna Mtore akianda mishumaa kwa ajili ya kuweka katika Kaburi la Baba yake.
Picha zaidi za Matukio ya Shughuli hii zinapatikana kupitia ukurasa wetu wa facebook, Tafuta 'Bukobawadau Entertainment Media' utapata pichazaidi na habari nyinginezo.
 Mh. Onesmo Niyegira ambaye ni Diwani Kata Buganguzi  akitoa utaratibu kulingana na ratiba
 Zoezi la kuweka mishumaa likifanyika kwa pamoja.
 Shughuli ya Mazishi ikiendelea...
 Mmoja wa waombolezaji akimfariji Ndugu Robart ( Mboma)Mtore ,ambaye ni Mtoto wa Marehemu
 Dada Oliva Lwebugisa mmoja wa waombolezaji.
 Mdau Wilbroad Revelian Mtore , Mmoja wa Watoto wa Marehemu Mzee Mtore.
 Kulia ni Mama Roderick Lutembeka.
Mdau Optay Henry pichani ameweza kushiriki Shughuli hii ya Mazishi.
 Kulia kabisa ni Mzee Rugalabamu(EDDEN)
 Anaonekana Mzee Abba pichani kushoto
 Mama Bandari , Ma Chalitina Mshana pichana kushoto akiteta jambo na Mama Muhazi.


Mdau Majid ( Kifedha) akiteta  jambo na Sheikh Hamada wa Kijijini hapo.
Katikati ni Bi Anna Revelian Mtore, Mtoto wa Mwisho wa kuzaliwa na Marehemu Mtore.
 Mzee Medad,Mkurugenzi wa Victorious Perch Hotel-Bukoba akiteta jambo na Mdau Willy Mtabuzi
 Mdau Avevan Tiba akimfariji Mdau Robart (Mboma) Mtore.
 Sehemu ya waombolezaji wakibadilishana mawazo baada ya Shughuli ya Maziko.
 Mdau Joha Rugenge, maarufu kama Rais wa Kanda ya Ziwa.
 Katika hili na lile baada ya Shughuli ya maziko anaonekana Mdau Wilbroad Mtore(Msouth
Wadau wakiwa bado msibani hapa kuwafariji wafiwa.
Sehemu ya waombolezaji.
Mmoja wa Wazee Kijijini Buganguzi
Taswira Jioni ya Leo June 27,2014 Shughuli ya Mazishi ya Marehemu Mzee Mtore
  Salaam zarambirambi kutoka Nchini Uganda kwa rafiki wa Karibu na Marehemu Mzee Reverian Mtore.

Mdau Mama Charles pichani
Moja ya Mti wa Kihistoria toka kizazi hadi kizazi uliopo Kijijini Katare-Buganguzi.
 Ndivyo inavyo onekana nyumba ya Milele ya Mzee wetu, mpendwa Wetu , Marehemu Mzee Raverian Mtore. 1934-2014
 Kiongozi wa Kiroho kutoka Parokia ya Rukindo akiagana na Mdau Wilbroad (Msouth) Mtore
 BUKOBAWADAU BLOG tunatoa pole kwa Familia ya Marehemu Mzee Reveria Mtore,ndugu,jamaa na marafiki 
 Tunamuomba MUNGU ailaze roho ya marehemu  pahali pema peponi amen!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau