Bukobawadau

MATUKIO YA PICHA ARGENTINA 3-2 NIGERIA

Mabao  mawili ya  Lionel Messi yanaiezesha Argentina kushinda dhidi ya Nigeria.
Dakika tatu za kipindi cha kwanza ,Messi pichani kulia anatupia bao la kwanza wavuni.1-0.
 Furaha ya Messi baada ya kuifungia Argentina bao la kwanza.
Mchezaji Messi pichani (kushoto), Di Maria (katikati) na Marcos Rojo wakishangilia bao la kwanza .
Asante Mola; Messi anaonyesha vidole  angani katika kushangilia baada ya bao lake la kwanza.
Ahmed Musa(kushoto) anapata bao la kusawazisha kuleta matumaini kwa Nigeria,katika ni Pablo Zabaleta akijaribu kuweka pingamizi ile hali ishapangwa kuwa hivyo.
Wachezaji wa Nigeria wanaungana na Ahmed Musa kushangilia  bao lake la kwanza
Furaha kubwa baada ya kufunga bao lake la kwanza la mchezo dhidi ya Argentina
Furaha ya wachezaji wa Nigeria ikiendelea baada ya kupata bao la kusawazisha.
Joseph Yobo anafurahi kwa kumbusu Mussa kwenye paji lake uso kufuatia bao lake la kwanza.
 Anaumia Mkono Mchezaji Michael Babatunde
Maumivu ya mkono yanapelekea Michael Babatunde kutolewa nje.
Kipa Vincent Enyeama akifanya awezavyo kumzuia Mshambuliaji Higuain.
Idadi ya Wachezaji wa Nigeria walivyozunguka kujaribu kumdhibiti  Mcheza nyota wa Barcelona, Messi
Mchezaji Sergio Aguero wa Argentina anaudhibiti  mpira dhidi ya Ogenyi Onazi wa Nigeria 
, pichani kushoto ni Mchezaji Ogenyi Onazi akikabiliana na Angel di Maria .
Messi anaipatia Argentina bao la pili.
Ni aina flani ya bao, ambalo huku kwetu ,kinyumbani wahaya wanasema ' Entonyeza'!!
Kushoto ni Mchezaji GARAY wa Argentina na Mchezaji Rojo pichani kulia wakimdhibiti mshambuliaji wa  Nigeria Peter Odemwingie 
Rojo (kushoto) akigonga kifua chake baada yakuipatia Argentina  bao la tatu na kuongoza 
Marcos Rojo (katikati) katika heka heka za kuifungia bao la tatu Argentina.
We ni Shidahh mzee umenichungulia mara mbili! Ndivyo anavyo onekani Kipa Vincent Enyeama wa Nigeria katika utani na Mchezaji Lionel Messi wa Argentina
Next Post Previous Post
Bukobawadau