Bukobawadau

BALOZI KAMALA ASHUKURU BENKI YA MAENDELEO YA ULAYA KWA MIKOPO NA MISAADA INAYOITOA KWA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP)

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akishukuru Benki ya Maendeleo ya Ulaya (EIB) kwa kutoa  mikopo ya gharama nafuu na kusaidia Maendeleo ya nchi za ACP. Balozi Kamala ameitaka Benki hiyo kuongeza kiwango cha mikopo inayotoa katika nchi za ACP kutoka asilimia 10 ya mikopo inayotoa sasa hadi asilimia 20. Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP leo imekutana na Uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Ulaya, Luxembourg kubadilishana mawazo jinsi ya kuboresha utendaji wa Benki na kuweka vipaumbele vya maendeleo na ushirikiano kati ya nchi za ACP na Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Next Post Previous Post
Bukobawadau