Bukobawadau

SHUGHULI YA MAZISHI YA MAREHEMU SULUM MOHAMED(SULUM ZERUZERU)LEO JULY 23,214

  Waumini wa dini ya kiislamu wakisalia mwili wa marehemu Sulum Mohamed maarufu kama (Sulum Zeruzeru) katika msikiti wa Jamia uliopo katikati ya Mji wa Bukoba,kabla ya kuupeleka makaburini jioni ya leo.
Swala ya Mwisho kwa Marehemu Sulum ikiendelea...
Waumini wa Kiislam wakikamilisha swala ya kuisalia maiti wakisalia maiti ya Marehemu Sulum.
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa Msikitinikatika kuuaga mwili wa Marehemu Sulum Mohamed.
Mwili wa Marehemu Sulum Mohamed (Sulum Bonge-Zeruzeru) ukiwekwa kwenye gari tayari kupelekwa eneo la makaburini lililopo Kishenge, ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba.
 Msafara wa watu na  magari wakiwa  barabara kuelekea eneo la Kishenge Makaburini
 Sehemu ya umati katika kusindikiza Mwili wa Marehemu Sulum aliyefariki Mchana wa leo Katika hospitali ya Mkoa wa Kagera baada ya kusumbuliwa na maladhi ya mara kwa mara.
Katikati linaonekana Gari aina ya Ambulance ikiwa imebeba mwili wa Marehemu Sulum Mohamed.
Mamia ya watu walioweza kushiriki shughuli ya mazishi haya.
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Sulum likitolewa kwene Gari
Hii ndiyo Safari ya Mwisho ya Marehemu Sulum (Bonge)Zeruzeru ,Allah amrehemu madhambi yake na Firdaus iwe makazi yake!
Sehemu ya wadau wakiwa eneo la makaburini kwajili ya kupokea jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sulum
 Maelfu ya watu wakiwa tayari eneo la makaburini
Taswira kutoka eneo la Makaburini Kishenge.
 Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna kichwabuta, Katikati ni Haji Mohammed, kuliani ni Ndugu Hussein Khalid.


Kushoto ni Ndugu Zacky Rajabal Visram na kulia ni Mzee Daudi Athman
 Mazishi yakiendelea.
 Ndugu Ibrahim Sokwala akishuhudia mwili wa marehemu unahifadhiwa katika makaazi yake ya kudumu
Katikati ni Uncle Majid Kichwabuta akishiriki kuustiri mwili wa marehemu Salum Mohamed.
 Zoezi la kuweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Sulum likiendelea
Anaonekana Ndugu Hafidhu Karugila (Nkurukumbi)Ndg Haruna Goronga katikati na Ndugu Majid Mzuzu
 Dua Maalum ya kumuombea Marehemu Sulum Mohamed 
 Sheikh Kakwekwe akiendelea na Dua ya kumuombea Marehemu katika hatua ya Mazishi.
 Ndugu Mandhu Sokwala pichani kushoto na Haji Gulam Rostamali pichani kulia
 Mzee wetu Haji Abbakari Galiatano katika kushiriki mazishi haya ya Marehemu Sulum Mohamed.
 Mwanazuoni katika taaluma ya Elimu na fani mbalimbali Mzee Ramadhani King.
 Pichani ni Mdau Abuba.
 Ndugu Dele wa Kahororo, Mdau Baruti na Abdallah wakiteta hili na lile.
Mdau Abdallah Idrisa 
 Taswira eneo la Makabulini ,shughuli ya maziko ikiendelea
Baada ya kumaliza dua na hiyo,Ndugu Salum Mawingo anatoa historia fupi ya Marehemu Sulum Mohamed aliyefariki mchana wa leo July 23,2014, majira ya Saa 8 Mchana,akiwa na umri wa miaka 56, Marehemu Sulum ameacha mjane na Watoto wanne.
Mwisho Sheikh Haruna Kichwabuta akitoa nasaha zake juu ya Umauti mara baada yashughuli ya mazishi haya.
 Timu nzima ya Bukobawadau Blog tunatoa pole kwa ndugu Jamaa na marafiki wa familia ya Marehemu Sulum Mohamed ,hakika hii ndiyo njia ya yetu wote ALLAH ampumzishe mahali pema peponi

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un!Next Post Previous Post
Bukobawadau