Bukobawadau

MISSENYI WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU

Dk Suleiman Mustapha wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania,mkoa wa Kagera akitoa maelezo ya kina kwa baadhi ya wachangiaji wa damu,kabla ya zoezi kuanza
Bango la huduma zinazotolewa hospitali ya Mugana
Muuguzi mfawidhi wa hospitali teule ya Mugana,sr Synthia Menezes(katikati)akishuhudia uchangiaji damu unavyoendelea.
Mwanachuo st Magdalena -Mugana,akichangia damu.
Sanstarius Skarion wa kata ya Bugandika(kulia)akitayarishwa na mtaalam wa Red cross kuweza kutoa damu
Rose Fortunatus(22)mwanachuo wa chuo cha uuguzi st Magdalena-Mugana,akipima uzito wake kabla ya kutoa damu
 John Msafiri wa Red Cross akionesha namna ya kusimama vizuri kwenye mzani il kupata uzito sahihi
NA MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi
WATANZANIA wametakiwa kujenga mazoea ya kuchangia damu ili kunusuru wagonjwa wanaoihitaji hasa wakati wa dharura.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na dk Suleiman Mustapha wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania,
mkoa wa Kagera wakati akiongea na wananchi waliojitolea kutoa damu na jamii kwa jumla,katika zoezi la uchangiaji damu lililofanyika hospitali teule ya Mugana wilayani Missenyi.

Alizitaja baadhi ya sifa za mtoa damu kuwa ni mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 65,mwenye uzito wa kuanzia kilo hamsini,na asiwe na magonjwa ya kifafa,shinikizo la damu,kisukari au upungufu wa kinga mwilini.

Muuguzi mfawidhi wa hospitali hiyo sr Synthia  Menezes alikuwa na matarajio kuwa watu wengi wangezitokeza kutoa damu kadri muda ulivyokuwa ukienda ingwa zoezi lilianza kwa kusuasua wakiwa wamejitokeza watu tisa wakiwemo wanachuo wa chuo cha uuguzi st Magdalena-Mugana,wahudumu wa wagonjwa na wengineo.
Mwisho


Next Post Previous Post
Bukobawadau