Bukobawadau

MSANII BEYONCÉ KUWANIA TUZO NANE MTV

Beyoncé anawania tuzo nane katika tuzo za MTV, ikiwemo video bora ya mwaka, msanii bora wa kike na unenguaji bora.
Wimbo wake Drunk in Love, alioimba pamoja na mumewe Jay-Z, unapambana na nyimbo kadhaa ukiwemo Happy wa Pharrell Williams katika video bora.
Tuzo hizo zitafanyika Inglewood, California Agosti 24.
Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza katika sherehe za tuzo hizo ni pamoja na Usher Raymond na Ariana Grade. Wasanii wengine watatajwa baadaye.
Wengine wanaowania tuzo ya video bora ya mwaka ni Miley Cyrus na wimbo wake Wrecking Ball, Chanderlier wa Sia na Fancy wa Iggy Azalea.
Next Post Previous Post
Bukobawadau