Bukobawadau

"NIMEMALIZA USAJILI" ASEMA MOURINHO

Boss wa Chelsea, Jose Mourinho amesema amemaliza kununua wachezaji msimu huu baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Filipe Luis kutoka Atl├Ętico Madrid.
Luis ni mchezaji wa nne mpya kusajiliwa na Mourinhomsimu huu baada ya Cesc Fabregas, Mario Pasalic na Diego Costa.
"Tumefunga biashara leo," amesema Mourinho. "Dirisha la usajili linafungwa Agosti 31, lakini sisi tumefunga Julai 19.
"Klabu yangu imefanya kazi nzuri, sio kwa wachezaji tulionunua tu, lakini pia kwa sababu tumemaliza biashara mapema kabisa."
Chelsea wamekuwa wakihusishwa na wachezaji kadhaa wa bei ghali msimu huu, akiwemo Sami Khedira wa Real Madrid na Radamel Falcao wa Monaco.
Next Post Previous Post
Bukobawadau