Bukobawadau

PITIA TETESI ZA SOKA ULAYA

Fabio Borini, 23, anajiandaa kujiunga na Sunderland baada ya Liverpool kukubali ada ya pauni milioni 14 (Sky Sports), baada ya kumchukua Filipe Luis siku ya Ijumaa, Chelsea wanazungumza na Atl├Ętico Madrid kuhusu kumsajili beki kutoka Brazil Joao Miranda, 29 kwa pauni milioni 20 (Daily Star), Real Madrid wanafikiria kumchukua Alvaro Negredo, 28, kutoka Manchester City kuziba nafasi ya Alvaro Morata, 20, anayekwenda Juventus (Metro), Liverpool wamemwambia Loic Remy, 27 kupunguza madai ya mshahara mkubwa kama anataka kufanikisha uhamisho wake wa pauni milioni 8 kutoka QPR (Daily Mirror).
 QPR wamepewa nafasi ya kumsajili Samuel Eto'o lakini huenda wakakataa kutokana na kutokubaliana mshahara (Daily Mail), Arsenal watakabiliwa na ushindani kutoka Valencia kumsajili kipa David Ospina, 25 (Metro), Everton wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili Romelu Lukaku, 21, kutoka Chelsea kwa uhamisho wa kudumu (Daily Mail), Tottenham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 10 wa beki Ben Davies, 21, kutoka Swansea.
 Liverpool pia walikuwa wakimtaka (Daily Telegraph), boss wa QPR, Harry Redknapp amesema anapanga kusajili wachezaji "sita au saba" zaidi kabla ya kuanza msimu mpya (Times), AC Milan wapo tayari kusubiri mwisho wa dirisha la usajili kuanza kumfuatilia Nani ambaye Manchester United wanataka euro milioni 14 (Corriere dello Sport)
Next Post Previous Post
Bukobawadau