Bukobawadau

SHULE YA MSINGI TUMAINI MANISPAA YA BUKOBA KUJENGWA UPYA KATIKA ENEO LA MAFUMBO KUPISHA UWANJA WA NDEGE BUKOBA

 Na: Sylvester Raphael
Habari njema kwa wananchi  wa Mkoa wa Kagera hasa wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Tumaini iliyopo katika Manispaa ya Bukoba  ambayo ipo upande wa Magharibi mwa  Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Shule hiyo  imepata mfadhili wa kuijenga upya katika eneo jingine kupisha uwanja wa ndege.
Habari njema hiyo ilitolewa na Mkuu wa mkoa wa Kagera katika Mkutano na waandishi wa Habari baada ya kuulizwa swali na waandishi hao kuhusu usalama wa wanafunzi na majengo ya shule hiyo kutokana na ndege kupita hatua chache sana toka angani wakati wa kutua jambo ambalo ni hatari kwa  shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa  Massawe  alisema mara baada ya uwanja wa Bukoba kujengwa katika kiwango cha lami Shule ya Msingi Tumaini ilianza kuonekana kuwa katika hatari hasa ndege kutimua vumbi kubwa kabla ya kuruka na kelele nyingi zinazosababisha watoto kutotulia wakati wakiendelea na masomo shule yao.
“Shule hiyo ipo karbu sana na uwanja wa ndege wa Bukoba na wakati wa ndege kutua hupita karibu sana  (hatua chache kutoka angani) jambo ambalo huleta taharuki kila mara ndege inapotaka kuruka au kutua , katika hali hiyo watoto hawawezi kusoma kwa amani na utulivu pia.” Alifafanua Mhe. Massawe.
Baada ya kuona kuwa ni tatizo kubwa na shule hiyo haiwezi kuendelea kuwepo eneo hilo Mkuu wa Mkoa  alipeleka wazo la kuhamisha shule hiyo kwa viongozi wa Benki ya Dunia ambao waliitembelea shule hiyo na kukubali kuijenga upya shule hiyo katika eneo linguine.
Benki ya Dunia watajenga Shule hiyo upya katika eneo la Mafumbo ambapo eneo lakujenga tayari limebainishwa na mara ya ujezi kukamilika majengo ya Shule ya Tumaini ilipo sasa yatabomolewa ili kuweka usalaama wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Katika Hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera ameendelea kuhimiza viongozi na wananchi kundelea kujenga maabara kila shule ya kata na kuzikamilisha maabara tatu kwa kila hule ifikapo mwezi Novemba 2014. Mpaka sasa mkoani Kagera zimejengwa maabara 62 kati ya 457, aidha majengo ya maabara ambazo hazijakamilika yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau