Sami Khedira hajasaini mkataba na klabu yake ya Real Madrid na yuko mbioni kuondoka.
KLABU ya Chelsea imepata nguvu ya kupambana kumsajili Sami Khedira baada ya jumatano usiku wakala wa mchezaji huyo kusema hakuna dili lolote lililokamilika na Asernal.
Kocha wa Blues, Jose Mourinho alimsajili beki wa kushoto Filipe Luis
jana kutokea klabu ya Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 18 na
sasa ametua nyavu zake kwa Mjerumani Khedira.
Ilifahamika kuwa
Arsenal wamekubaliana ada ya uhamisho ya paundi milioni 20 na Real
Madrid ili kuinasa saini ya nyota huyo mwenye miaka 27, lakini walikuwa
wanahangaikia suala la mshahara ambapo mchezaji huyo anahitaji paundi
laki moja na elfu themanini kwa wiki.
Hata hivyo, wakala wa
Khedira, Jorg Neubauer alisema: “Hatuko kwenye mazungumzo na Arsenal.
Sidhani kama makubaliano ya ada yanaweza kufanyika, vinginevyo ningekuwa
nimeambiwa.”
“Khedira anapendwa na Mourinho tangu wakati huo yupo
Real Madrid na kocha huyo anaeleweka hivyo. Hilo pia limehamia akiwa
Chelsea”.
Khedira yupo tu kutokana na wawakilishi wa Real Madrid na mchezaji kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mktaba.
Neubauer aliongeza: “Tupo katika mzungumzo na Real Madrid kuhusu
mkataba, lakini hakuna kinachokaribia kuamuliwa. Sami amerudi kutoka
kombe la dunia na amekwenda likizo”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment