Bukobawadau

WANAHABARI KAGERA WAPONGEZWA KWA UMOJA WAO

Mwenyekiti wa KPC,John Rwekanika wakati  akifungua mkutano huo mkuu wa waandishi wa Habari Kagera.
 Baadhi ya waandishi waliohudhuri mkutano mkuu
Mwekahazina wa KPC,Lilian Lugakingira akifafanua masuala ya fedha kwenye mkutano huo
Junior Mwemeziwa Azam TV,akichangia kwenye mkutano huo.Waliokaa kushoto kwake ni Winifrda Simon na Meddy Mulisa
Kutoka kulia ni katibu wa KPC,Phinias Bashaya,mwenyekiti-John Rwekanika na mwekahazina Lilian Lugakingira
Katibu wa KPC,Phinias Bashaya akisoma kumbukumbu za mkutano mkuu uliopita
NA MUTAYOBA ARBOGAST,Bukoba
WITO umetolewa kwa waandishi wa habari mkoani Kagera ambao ni wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani hapa (KPC) kudumisha umoja na maelewano waliyonayo ili kuifanya klabu yao kuwa na nguvu zaidi.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa klabu hiyo,John Rwekanika wakati akifungua mkutano mkuu wa wanachama mwishoni mwa juma katika ukumbi wa Lake Hotel mjini Bukoba.

Alisema kuwa KPC imekuwa klabu ya kupigiwa mfano hapa nchini miongoni mwa vilabu vya habari zaidi ya 25 kwa kusuluhisha migogoro yake ya ndani  na kuwa sasa klabu hiyo inao mshikamano mkubwa,ingawa changamoto kama kutolipa ada kwa wakati ,hazikosekani.
Ili kujenga demokrasia na haki  ndani ya klabu kama yalivyo maelekezo kutoka muungano wa vilabu vya habari Tanzania(UTPC),klabu hiyo imeundakamati ya uchaguzi wa viongozi wake utakaofanyika kati ya Januari hadi Mei 2015.


Kwa hali hiyo ili kuweka uwazi katika mchakato wa uchaguzi. Wajumbe wa kamati hiyo wanatakiwa kuwa ni wale tu ambao wanaona hawatashiriki katika kugombea nafasi mbalimbali,na kuwa kamati hiyo itavunjwa mara baada ya utaratibu mzima wa uchaguzi kukamilika ikiwamo kusikiliza na kuamua juu ya rufaa kama zitakuwepo.


Waliochaguliwa ni Meddy Mulisa,Arodia Dominick,Winifrida Simon na Pontian Kaiza.
Mkutano huo mkuu umeagiza majina yote 13 ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wanaofanya kazi mkoani Kagera,walioomba kujiunga na KPC,yajadiliwe kwanza na kamati tendaji kabla ya kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu kwa uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa katiba.
Aidha mkutano huo uliona kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuwasaidia na kuwajulia hali waandishi wa habari waliokuwa wanachama wao lakini sasa hawako kazini kutokana na kuugua kwa muda mrefu ambao niBenjamini Rwegasira na Raymond Owamani.
Next Post Previous Post
Bukobawadau