Bukobawadau

WAWEKEZAJI WAANZA KUITIKIA WITO WA KUWEKEZA MKOANI KAGERA

Na, Sylvester Raphael
Mkoa wa Kagera umekuwa ukifanya juhudi  kabambe  za kujitangaza na kuzitangaza  fursa zake mbalimbali za uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza mkoani humo kwa nia ya kuinua pato la mkoa pia kuinua uchumi  wa  wananchi kupitia ajira.
Juhudi hizo za mkoa wa Kagera zimeanza kuleta matumaini baada ya wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuanza kuonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo cha kibiashara na kisasa pamoja na ufugaji wa ng’ombe wa kisasa.

Global International Agency ni Kampuni mojawapo ya ndani ya nchi ambayo imeonyesha nia ya kuja kuwekeza mkoani Kagera katika sekta ya kilimo cha kisasa cha kibiashara  katika zao la shairi ambapo tayari kampuni hiyo imeshapata maeneo ya kuanzia kilimo hicho katika  wilayani Missenyi.

Kampuni ya Global International Agency tayari imefanya utafiti wa kutosha katika mkoa wa Kagera kuhusu ustawi wa zao la shairi na imeonekana hali ya hewa pamoja na aina ya udongo vinafaa sana kustawisha zao la shairi.
 Utafiti huo umefanywa katika Wilaya Missenyi na tayari maeneo ya kulima zao la shairi ya mepatikana katika kata ya Bugolola kwenye vijiji vya Bugolola, Buchulago na Kabingo pia kata ya Mushasha katika kijiji cha Bulembo.

Global International Agency baada ya kupata maeneo hayo katika Wilaya ya Missenyi inaendelea na utafiti katika maeneo mengine ya mkoa wa Kagera ili kupata maeneno mengi zaidi. Aidha inaendelea na utafiti jinsi ya kushirikisha wananchi katika kilimo hicho kwa kuwanufaisha bila kuwanyonya.

Akiongea katika kikao na uongozi wa mkoa wa Kagera Kuhusu soko la shairi Mkurugenzi Mtendaji wa Global International Agency alisema kuwa zao la shairi lina soko kubwa kwani pamoja na kutumika kutengeneza pombe (Beer) lakini plastiki kama chupa za maji na ndoo pia mabaki hutengeneza kartasi.

“Tanzania Breweries Limited (Kampuni ya kutengeneza Bia Tanzania TBL) inapata asilimia 25 ya shairi kutoka Tanzania na asilimia 75 ni kutoka nje ya nchi jambo ambalo linaonyesha uhuhitaji shairi katika soko.” Alisistiza Fidelis Bashasha Mkurugenzi Mtendaji Global International Agency.

Uwekezaji katika kilimo cha shairi mkoani Kagera utfungua fursa nyingine nyingi katika uwekezaji kutokana na zao la shairi kutengeneza vitu vingi kama plastiki mfano chupa za maji, ndoo, viti na beseni.  Aidha masalia yake hutumika kutengeneza karatasi pia shairi hutumika kutengeneza chakula kama mikate.

Kutoka na hali hiyo kilimo cha shairi kikifanikiwa mkoani Kagera wawekezaji wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za plastiki watakuja kuanzisha viwanda hapa mkoani Kagera kikiwemo kiwanda cha kutengeneza karatasi kwani malighafi itakuwa inapatikana kwa urahisi.

Kampuni ya Global Internationa Agency wanahitaji hekari 100,000 za ardhi ili kuzalisha  zaidi ya tani 100,000 za shairi ili kukidhi soko la ndani nje ya nchi. Pia uwekezaji mara utakapoanza wananchi 8700 wanatarajia kupata ajira kwa kuanzia.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Richard Kwitega aliipongeza Kampuni ya Global International Agency kwa kukubali kuwekeza katika mkoa wa Kagera na kuwaomba pia wasiishie katika wilaya moja ya Missenyi bali wazifikie Wilaya zote za Mkoa wa Kagera.


Next Post Previous Post
Bukobawadau