Kwenye
mkutano na waandishi wa habari leo, Dodoma Hotel, Mjumbe wa Kamati ya
Chama na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao ametoa kauli
nzito akisema atakuwa mtu wa mwisho kusaliti CHADEMA na siasa za
mabadiliko kwa ujumla.
Abwao
ambaye ni mmoja wa akina mama shupavu na imara wa CHADEMA akiwa
ametumikia Watanzania kwenye siasa za mabadiliko tangu miaka ya mwanzo
ya mfumo wa vyama vingi, amesema hawezi kwenda kinyume na maamuzi ya
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umeazimia kusimamia maoni ya
wananchi kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.
Mbunge
huyo amelazimika kuweka kumbukumbu sawa mbele ya mkutano na waandishi
wa habari, baada ya kuwepo taarifa za upotoshaji kuwa yuko Mjini Dodoma
kushiriki vikao vya Bunge Maalum la Katiba Mpya vinavyoendelea mjini
humo.
"Hizi
ni mbinu za kitoto za kutaka kuniharibia jina langu na kazi zangu za
kisiasa. Mimi Chiku Abwao nitakuwa mmoja wa watu wa mwisho kabisa
kukisaliti chama changu...nitakuwa mmoja wa watu wa mwisho kabisa
kusaliti mageuzi na mabadiliko ya mfumo na utaawala ambayo nimeyapigania
sehemu kubwa ya maisha yangu.
"Natambua
msimamo wa kuwataka wabunge na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
wanaotokana na chama chetu kutohudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba
Mpya ni azimio la Kamati Kuu ya Chama ambayo mimi pia ni mjumbe, siwezi
kukiuka maagizo ya chama.
"Chama
kupitia Kamati Kuu kiliazimia kwamba wajumbe wanaotokana na CHADEMA
tutaungana na wenzetu wengine kwenye UKAWA kutohudhuria vikao vya Bunge
Maalum kwa sababu hakuna nia ya dhati ya kutafuta maridhiano ya kitaifa
katika mchakato huu kwa kujadili maoni ya wananchi bungeni.
"Mimi
siwezi kuja hapa Dodoma kusaliti UKAWA na kushiriki vikao vya Bunge
Maalum la Katiba...maamuzi ya UKAWA ni maamuzi ya wananchi, siwezi kuja
hapa kuwasaliti wananchi. Ninajua ninachokifanya katika siasa za
mageuzi, ni kutumikia wananchi si kutafuta maslahi," amesema Abwao.
Abwao
amezidi kufafanua kwamba aliwasili Dodoma kwa ajili ya kuchukua gari
yake aliyoiacha katika yard ya bunge wakati alipoondoka nchini kwenda
Australia akiwa sehemu ya ujumbe wa Bunge, kuiwakilisha nchi kwenye
mkutano wa masuala ya UKIMWI.
Amesema
kuwa alipofika mjini Dodoma alikwenda kulichukua gari lake kwenye yard
ya bunge (viunga vya bunge) na akaanza kulifanyia matengenezo kwa ajili
ya safari ya kwenda Iringa.
"Siku
ya jana (Jumatano) nimekuwa na kazi ya kuzunguka hapa mjini kutafuta
spares kwa ajili ya kutengeneza gari langu...sasa nimeonekana sana huko
kwa sababu nilikuwa natumia usafiri wa taksi...wao wakaamua kufanya
propaganda za kwamba mimi niko hapa kuhudhuria Bunge Maalum. Wanapoteza
muda wao. Tuko na wananchi," amesema Abwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment