Bukobawadau

KARAGWE YETU KWA MUHTASARI

 Taswira mji wa Kibiashara Omurushaka Wilayani Karagwe
 Tunapozungumzia historia ya watu wa mahali fulani hatuna budi kuzungumzia Jiografia ya sehemu husika, hali ya hewa na mazingira , wakazi wake ,uoto wa asili ,utamaduni wao ,utawala ,mawasialiano na uchumi ..
  Lengo la kutafuta na kuifahamu vyema historia ya watu wa Karagwe ni la msingi sana. Lengo kuu ni kuandaa mazingira ya watu mbalimbali  ili waweze kuielewa vyema  historia ya Karagwe, kukusanya na kuzihifadhi zana na kumbukumbu za kimila na jadi ambazo katika siku za karibuni zinaelekea kuanza  kupotea. Makala hii itachambua kwa kina historia ya kabila la Wanyambo ambao kwa asili wanatoka Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera
 Jina “ Karagwe “ kutokana na simulizi za wazee wetu mbali mbali na watafiti wa historia ya Karagwe  kama ( Katoke 1975; 162) inaelezwa kwamba  jina hili linatokana na kilima (angalia kielelezo hapa chini) kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao makuu ya wilaya  ya Karagwe ,kwenye kijiji cha Kandegesho ,kata ya Nyakakika ambacho mtawala ( Omukama ) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza. Taarifa zilizopo mtawala huyo alijulikana kwa jina la Nono ya Malija kutoka ukoo wa Basiita. Na kwamba kumbukumbu hii ya “Karagwe ka Nono “inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia wa Karagwe kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara. Inasemekana kwamba Nono son of Marija alikabidhi madaraka yake bila ya misukosuko wala mapigano ya aina yoyote kwa ajili ya kuokoa watu wake waliokuwa wanakabiliwa na wimbi la njaa. Kwa kifupi hii ndio kumbukumbu yake na chimbuko la historia ya jina Karagwe.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa wakati Omukama Rumanyika Orushongo anaingia madarakani, Karagwe ilikuwa tayari imekua kiuchumi kiasi ambacho wafanyabishara toka maeneo ya mbali walikuwa wameanza kuingia Karagwe wakifanya biashara ya meno ya tembo, mazao ya chuma (Iron products) kama vile visu, majembe na vitu vingine wakibadilishana na bidhaa waliyoleta toka maeneo waliyotoka.
Mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni mwa karne ya 19, habari za kushamili
kwa Karagwe kutokana na biashara zilikuwa zimesambaa sehemu mbalimbali  za nchi ya Tanganyika pamoja na nchi za jirani za Rwanda, Kongo, Uganda, Burundi na hata nchi za Falme za Kiarabu. Wakati huo Karagwe ilikuwa imekwishatembelewa na wajasiliamali toka Unyamwezini na Usumbwa ambao walileta chumvi toka Uvinza na chuma toka Katanga (nchini Kongo) .

Hili linathibitishwa na msemo wa kinyambo wa muda mrefu unaosema “Omwonyo ngunula, chonka Omushumbwa nanunka”kwa kiswahili maana yake ni kwamba chunvi yao ni tamu pamoja na kwamba wachuuzi wenyewe wanatoa harufu mbaya ya jasho tokana na safari yao ndefu.
Wilaya ya Karagwe na ile ya Kyerwa bado ina ardhi yenye rutuba inayostawisha mazao mengi ya ya kilimo na ufugaji ambayo bado haijatumika ipasavyo. Wakulima wengi katika wilaya hii wanalima kilimo na kufuga kienyeji bila ya kutumia utalaam kuzalisha kwa wingi. Mazao kidogo yanayozalishwa ndio yanasafirishwa kwenda mikoa mingine yanayoifanya Karagwe kusifika. Mazao ya mifugo (Ngozi, maziwa na pembe za ng’ombe) nayo bado hayajatumika vyema, hatuna viwanda vya kusindika mazao hayo.
 Kila mmoja wetu anajua kuwa wilaya zetu za Karagwe na Kyerwa zinategemea sana kilimo kwa ajili ya chakula na biashara ,lakini mito mingi na mabonde tuliyo nayo haijatumika vyema kuongeza uzalishaji wa chakula . Ili kuinua kipato cha wananchi wa wilaya hizi kuna haja kubwa kwa Halmashauri zetu kutenga bajeti na kuhimiza wananchi kutumia kilimo cha umwagiliaji.
 Katika wilaya hii eneo la Kibanda huko Bugomora lilikuwepo shamba la NAFCO na lilikuwa na uwezo wa kuzalisha ngano bora kuliko eneo lolote hapa nchini, eneo hili halitumiki. Tunaweza kufufua shamba hili kama tutakuwa na nia.
 UTAWALA  NA WATAWALA  WA KARAGWE
Kama ilivyokwishaelezwa hapo juu mtawala wa kwanza wa Karagwe alijulikana kwa jina la Nono ya Malija , Ruhinda alipofika Karagwe kutoka kusini alimkuta mtawala huyu mwenyeji  ambaye alilazimika kuachia madaraka yake na kumpisha Omukama  Ruhinda ili kuokoa watu wake waliokuwa wanakabiliwa na njaa wakati huo.
 Ruhinda baadae alijenga Boma lake eneo la Bwehange eneo lililopo  kusini mwa  ziwa Kajunju ambalo baade lililobatizwa na Bwana Speke “The little Windemere” akiwa na maana ya kuwa lilifanana sana na ziwa Windemere linalopatrikna nchini Uingereza ,na baadae Omukama Ruhinda aliweza kuhamia Bweranyange, mahali palipo karibu na uwanda wa juu penye mtelemko wa vilima vinavyozunguka ziwa hili .Hapa ndipo watawala wote waliofuatia waliopotawalishwa hadi walipofika wadachi. Inaelezwa kuwa hakuna msukosuko mkubwa uliotokea wakati wa utawala wa Omukama Ruhinda, na inasemakana alitawala watu wake kwa haki na utulivu kwa miaka mingi.
 Omukama Ruhinda alirithiwa na mwane Ntare mwaka 1800, wakati huo kulitokea mashambulio ya Wanyoro katika Karagwe na kwa vile Omukama Ntare alikuwa bado mdogo alikimbia na mama yake,  akabaki wakili wake ambaye pia aliuawa na Wanyoro.  Baadae wanyoro walishambuliwa  na ugonjwa mbaya ambao unasemekana kuwa ulitokana na uchawi wa Ntale aliopewa na Mfalme wa Uha (Buha –Kigoma)  na wakati anarudi na mama hakukuta mnyoro hata mmoja kwani wale ambao hawakufa walikimbia kwa woga. 
 Mfalme Ntare alifuatiwa na Ruhinda VI ambaye maisha yake yalikuwa marefu sana hata mwisho watu kuamini kwamba hatakufa. Omukama Ruhinda VI aliamua kujiua mwenyewe ili kumpisha mwanae Ndagara ili atawale , Ndagara alikuwa shujaa wa vita alipigana vita na Kiziba ,Kyamtwala na Ihangiro .Hakuna ushahidi wa kutosha lakini mara zote simulizi za wazee wanyambo husema Ushindi katika vita hii ulikuwa wa kwao!!.
 Ndagara alikufa mwaka 1855 na mwanae Rumanyika alitawazwa kuwa mfalme wa Karagwe kabla ya kukutana na Bwana Speke mwaka 1861.

 Muonekano wa Jengo la Hpspital ya E.L.C. T Nyakahanga.
 Mazingira ya safi y Hospital ya Nyakahanga iliyopo Omurushaka Wilayani Karagwe.
Bukobawadau Blog tunatoa Credit Kubwa kwa ndugu Livingstone Byekwaso kwa maneno ya kihistoria kuhusu KARAGWE NA WATU WAKE (WANYAMBO).
 UTAWALA  NA WATAWALA  WA Karagwe

Kama ilivyokwishaelezwa hapo juu mtawala wa kwanza wa Karagwe alijulikana kwa jina la Nono ya Malija , Ruhinda alipofika Karagwe kutoka kusini alimkuta mtawala huyu mwenyeji  ambaye alilazimika kuachia madaraka yake na kumpisha Omukama  Ruhinda ili kuokoa watu wake waliokuwa wanakabiliwa na njaa wakati huo.

 Ruhinda baadae alijenga Boma lake eneo la Bwehange eneo lililopo  kusini mwa  ziwa Kajunju ambalo baade lililobatizwa na Bwana Speke “The little Windemere” akiwa na maana ya kuwa lilifanana sana na ziwa Windemere linalopatrikna nchini Uingereza ,na baadae Omukama Ruhinda aliweza kuhamia Bweranyange, mahali palipo karibu na uwanda wa juu penye mtelemko wa vilima vinavyozunguka ziwa hili .Hapa ndipo watawala wote waliofuatia waliopotawalishwa hadi walipofika wadachi. Inaelezwa kuwa hakuna msukosuko mkubwa uliotokea wakati wa utawala wa Omukama Ruhinda, na inasemakana alitawala watu wake kwa haki na utulivu kwa miaka mingi.
 Omukama Ruhinda alirithiwa na mwane Ntare mwaka 1800, wakati huo kulitokea mashambulio ya Wanyoro katika Karagwe na kwa vile Omukama Ntare alikuwa bado mdogo alikimbia na mama yake,  akabaki wakili wake ambaye pia aliuawa na Wanyoro.  Baadae wanyoro walishambuliwa  na ugonjwa mbaya ambao unasemekana kuwa ulitokana na uchawi wa Ntale aliopewa na Mfalme wa Uha (Buha –Kigoma)  na wakati anarudi na mama hakukuta mnyoro hata mmoja kwani wale ambao hawakufa walikimbia kwa woga. 

Mfalme Ntare alifuatiwa na Ruhinda VI ambaye maisha yake yalikuwa marefu sana hata mwisho watu kuamini kwamba hatakufa. Omukama Ruhinda VI aliamua kujiua mwenyewe ili kumpisha mwanae Ndagara ili atawale , Ndagara alikuwa shujaa wa vita alipigana vita na Kiziba ,Kyamtwala na Ihangiro .Hakuna ushahidi wa kutosha lakini mara zote simulizi za wazee wanyambo husema Ushindi katika vita hii ulikuwa wa kwao!!.

Ndagara alikufa mwaka 1855 na mwanae Rumanyika alitawazwa kuwa mfalme wa Karagwe kabla ya kukutana na Bwana Speke mwaka 1861.

Watawala wengine waliotawala Karagwe walikuwa kama ifuatavyo;Ruhinda I
Ntare  Ruhinda II, 1550 Ntare II   ,   1575  Ruhinda III, 1595 Ntare III ,1620 Ruhinda IV    1645  Ntare IV, 1675 Ruhinda V  1700 Rusatira   ,1725 Mehiga ,1750 Kalemera ,1775 Ntare V (Kiitabanyoro) ,1795 Ruhinda Orushongo ,1820 Ndagala I,1853 Rumanyika I
 1883 Kayenje Kalemela,   1886 Ndagala II ,1893 Ntare VI,1916 D.Rumanyika II
1939 B.I.Ruhinda VII –The last Muhinda ruler of Karagwe
1963 End of political power of traditional rulers in Tanzania.

Next Post Previous Post
Bukobawadau