YAH: KUTOSHIRIKI AWAMU YA PILI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA.
Mtakumbuka
kuwa Chama chetu kwa kushirikiana na vyama vingine vinavyoounda Umoja
wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) tuliamua kutoka katika Bunge maalum la
Katiba baada ya CCM kuamua kukiuka utaratibu wa mchakato wa kupata
katiba mpya kama ulivyoainishwa katika sheria ya mabadiliko ya Katiba na
kuweka Mkakati wa kupitisha Rasimu ya CCM ya serikali mbili.
Pamoja na juhudi ambazo tumeendelea kuzifanya kama Chama na UKAWA, hadi
sasa bado CCM wanaonekana hawana dhamira ya dhati ya kuurejesha mjadala
wa Katiba Mpya kwa kuheshimu maoni ya wananchi kama yalivyoratibiwa na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuwekwa katika Rasimu ya Katiba
iliyowasilishwa katika Bunge Maalum.
Kwa barua hii, Wabunge
wote wa Bunge Maalum la Katiba tunaotokana na Chama cha CUF tunajulishwa
kutokwenda kushiriki katika kikao cha awamu ya pili ya Bunge hilo
kinachotarajiwa kuanza tarehe 05/08/2014. Kama Chama kinachoheshimu
Demokrasia ya kweli, hatuwezi kushiriki na kuvipa uhalali vikao vya
Bunge Maalum vyenye lengo la kuyapuuza na kuyatupilia mbali maoni ya
Wananchi.
Nawatakia kila la heri,
HAKI SAWA KWA WOTE
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
sisi kama wananchi tuliowatuma kwenda dodoma kushirik katik huo mchakato hatukuwatuma huko kutoka bungeni kwani tulijua fika kwamba jambo mnaloenda kulifanya ni jambo muhimu la mhimili wa taifa letu hivyo mlitakiwa kupambana na hoja yakinifu ili kuonesha nguvu za watanzania tuliowatuma hivyo hatukubaliani na hoja yenu ya kususia vikao vya bunge maalum la katiba ambalo sio maslahi kundi fulani fulani
Post a Comment