Bukobawadau

SAKATA LA EMMANUEL OKWI

UNAWEZA kurudia kusema kweli hii sasa ni vita, kwani uongozi wa klabu ya Yanga, umelihamishia suala la kesi ya Emmanuel Okwi kwenye kamati ya sheria ya klabu hiyo ambayo ina watu 16.

Pamoja na wanasheria hao 16, taarifa za uhakika zimeelezwa Yanga inaunganisha mwanasheria mmoja kutoka Uswisi yaliko makao makuu ya Fifa ambaye atafanya kesi hiyo kuunganisha wanasheria 17 wa nchi mbili tofauti.
Kamati hiyo ambayo ina wiki moja tu tokea itangazwe, inaundwa na wanasheria mahiri wakiwemo maprofesa wawili, daktari mmoja wa sheria pamoja mawakili zaidi ya 10.

Timu ya wanasheria 16 wanaounda ‘kikosi’ cha kamati ya sheria ya Yanga ni hawa wafuatao, Profesa Mgongo Fimbo, Gikas Farija, Jessica Kabisa, Profesa Mpalamaganda Kabudi, January Kambamwene, Herman Lupogo, Richard Madibi, Burton Mahenge, Alex Mgongolwa, Elisha Mkucha, Mudhihir Mudhihir, Saleh Njaa, Tausi Abdallah, Cathbert Tenga, Dk Ringo Tenga na Audax Vedasto. 

Source: CHAMPION .
Next Post Previous Post
Bukobawadau