Bukobawadau

SALAMU YA BEN MULOKOZI 'HATA KAMA HAJAKWAMBIA'

Hata kama hajakwambia, haimaanishi hakimuumi, yamkini ameamua kunyamaza kimya maana anajua fika kwamba akiamua kumwambia utabisha, utapinga, utakataa, utajitetea, utaruka kabisa, unaweza hata kumpiga au kumtukana, au kumwuona yeye ndiyo mkosaji na kumlazimisha yeye ndio akuombe msamaha badala ya wewe kuomba msamaha, ila fahamu fika ya kwamba anaumia hata kama hajakwambia, na kutokukwambia kwake hakumaanishi kwamba anaridhika, anafurahi au haoni uchungu wowote, la hasha, anaumia sana, tena sana tu, lakini ameamua kunyamaza.
 Ni bora ukalifahamu hili sasa ukajitahidi kuliokoa penzi lako kuliko ukachelewa na kumkosa mwana na maji ya moto .
Hii ni Salamu ya leo Jumanne kutoka kwa Mr. Ben Mulokozi aka mr.appetizer pichani.
Pichani kushoto ni Mr. Basibila na kulia ni kijana wake Ndugu Bushira.
Mr.Ben Mulokozi aliyepo mjini hapa kwa siku ya tatu ikiwa ni ziara maalumu kwa ajili ya kukagua miradi yake mbalimbali.Ikiwa amejikita zaidi katika kilimo huko Kagera Sugar Wilayani Missenyi tayari anayo mashamba ekili 300 .

Mdau Ben Mulokozi  Yeye kama Real Estate  'property deals' aka (Binuzi) anawahasa  Wadau mbalimbali wajaribu kuwekeza Nyumbani ,anawataka watu wawekeze zaidi katika kilimo .'
Mwisho anasema;'mbalikiwe nyote mtakao nielewa'!!
Victoria Perch hotelni hoteli ya kisasa iliyo katika viwango vya hali ya juu  hoteli inatoa huduma nzuri ya vyumba vya kulala,vyakula
 Ndani ya Ofisi za World's first computer ,wauzaji na watengenezaji wa Computers na Laptop za kisasa pamoja na vifaa mbali mbali nakutana na Mtaalam Ndugu Mwinyi Six pichani.
 Taswira Vilima vya Kashabo-Bukoba.
Barabara ya Jamhuri Mjini Bukoba.
 Camera yetu inakutana na Mdau Edgar 'Diggar Daz' katika mitkasi ya kimjni 
 Ile tu naondoka naelekea Mitaa ya Kati Mjini hapa  mwanalibeneke nakutana na kitu ingine...... 
Ni nwanadada Zakia 'Zachybby' Kassimu ni shabiki na mpenzi wa libeneke la Bukobawadau Blog.
 Kijana Anaf Hamad akiwajibika.
 ELCT Ujirani mwema.
 Mama Litta  pichani akiwa ndani ya Duka lake linalojishughulisha na uuzaji wa nguo,viatu,mikoba na vitu vya mitindo mbalimbali ya fashion, Wapo Mkabala na jengo la 'Ujirani Mwema'
Mbele yaCamera yetu ni Bibie Laty,hapa ni makutano ya 4 Ways,akielekea Dukani kwa Mama Litta.
Heka heka za Vijana wa Mjini pichani ni Abdulnasal 'BudaNasy' Kangezi na Idd Mabrouk 'Seaman'


Next Post Previous Post
Bukobawadau