SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

17 September 2014

TAARIFA YA MWANAFUNZI WA IHUNGO ALIYEJINYONGA

Mwanafunzi wa kidato cha TANO katika shule ya sekondari ya IHUNGO, EZERA WABAMBA aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa KAGERA, amejiua kwa kujinyonga na shuka kwa madai ya kukosa huduma sahihi za matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA, GILLES MUROTO amesema marehemu kabla ya kujingonga aliandika ujumbe uliokutwa kwenye mwenye mwili wake ambao ulipatikana baada ya maiti yake kufanyiwa upekuzi akieleza sababu zilizopelekea ajinyonge.

‘ujumbe huo ulisema haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama mbwa ,huku akisema amepewa dawa bila kufanyiwa vipimo’

Kwa upande wake katibu wa hospitali hiyo JUSTUS BENGESI ambaye amethibitisha taarifa za kifo cha Mwanafunzi huyo, amesema si kweli kwamba amefikia uamuzi wa kujinyonga baada ya kukosa huduma sahihi za matibabu,na kuwa alifanyiwa vipimo vyote na kubainika akisumbuliwa na ugonjwa wa MALARIA.
Mwanafunzi huyo aliyejinyonga mwenye umri wa miaka 19 alikuwa mzaliwa wa TABORA na alikuwa akisoma mchepuo wa masomo ya SAYANSI.

3 comment:

Anonymous said...

Poleni wafiwa,

Naomba viongozi wa taasisi mbalimbali tuache mara moja taharifa za kukanusha kila matukio mazito kama haya yanapotokea. Ukilitazama hili tukio ni lazima kuna uzembe wa namna moja au nyingine ulijitokeza hadi kufikia hatua ya kijana huyu kukata tamaa. Najua yeyote anaweza kutengeneza chochote kama ushahidi wa vipimo vya huyu kijana ili kujinasua na hili tatizo ila ukweli ni kwamba sote tunafahamu hili tatizo lipo hapa nchini kwetu, kama huna pesa ya kumpa doctor hupati huduma, ndugu zetu wengi wamepitia na sisi wenyewe na bado tunaendelea kuteseka, ni mara ngapi kina mama wajawazito wanateswa hadi wengine kutukanwa na manesi wetu mambo ya ajabu na ghafla kitoto kichanga kinadondoka sakafuni?
Uongozi wa hospital ya mkoa wa Kagera mnayo mengi ya kujibu ni kwanini huyu kijana ameamua kujiua na kuandika ujumbe huu na sio kukimbilia kuwa alikuwa na malaria, au mnataka tuamini kuwa malaria ilimpanda kichwana na akachanganikiwa na kuwa kichaa? Na kama ni kichaa basi cha kwake ni kizuri kwani ameweza kuandika mambo ya ukweli na mazuri ya kukufungueni macho. Wafanyakazi wote waliokuwa zamu siku anakuwa admitted hadi siku ya kufa lazima wawajibike, na uongozi ni lazima uwajike kwa hili. Utaueleza nini uma mgonjwa anafikia hatua ya kujinyonga hadi kufa katika eneo la hospital bila kuonekana na mtu yeyote? Au nyote mlikwenda kunywa Rubisi?

Jamani ndugu zangu badilikeni hizo kazi kama hamna wito nazo acheni nenda mkalime au kavue samaki kuliko kutuymiza.

Kazi kukaa tu kwenye vikao vya harusi na birthday party zisizo kuwa na tija, mara oh bukoba club n.k.

Inywe bahaya ba Bukoba tweshubeho, obufela, ekiburi ne eirangira lyaijakutwita.Burula mmbone abandi nibairuka inywe nimwajula nka butono.
hmmmfuuu ngu barangira biki si!!!!

Asanteni sana,
Ndugu yenu aliyochoshwa na ujinga wenu huu, kila siku kutumiwa tu no okukurata abanasiasa na abainamu esenti ahanyo nke embwa.

Anonymous said...

baraka mbona umeibania comment yangu niliyotuma juu ya hili swala?

Unknown said...

Sasa hapo,nadhani wote tunaweza kukubaliana na Hayati,mwalimu Julius.K. Nyerere kuwa,adui mmojawapo wa maendeleo ya Watanzania,ni maradhi;maana,mwanafunzi huyo ambaye alikuwa anasoma sayansi,angeweza kuwa daktari labda,au enginere au katibu wa Hospitali,lakini sasa adui maradhi,amemtesa kiasi cha kuamua kujiua,na KATIBU anasema sijuhi nini na nini na nini na nini,aha!mambo haya hadi yanatia kinyaa:R.I.P mwalimu J.K.Nyerere!

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU