BALOZI KAMALA AMKABIDHI CHETI CHA UTAMBUZI BWANA SAITOTI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji ya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili
Kutoka kulia) akimkabidhi cheti cha utambuzi Bwana Saitoti kumshukuru
kwa kazi nzuri anayofanya ya kutafuta fedha Ubelgiji ya kusaidia
kupambana na Umaskini Handeni Tanzania. Bwana Saitoti ametafuta fedha za
kusaidia kutekeleza miradi ya maji Handeni. Balozi Kamala amekabidhi
cheti hicho leo Ubelgiji- Antiwerpen. Balozi Kamala amesema kila mwaka
Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji utakuwa unatoa vyeti mbalimbali vya
kutambua kazi nzuri zinazofanywa na Asasi Zisizo za Kiserika za kutafuta
fedha ya kusaidia kutekeleza miradi mbalimbali Tanzania.