Bukobawadau

KAMPUNI ZA UINGEREZA ZAINGIA TANZANIA

Ujumbe wa makampuni 14 ya biashara za aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na sekta za elimu na mafunzo, ulinzi, ushauri elekezi na afya kutoka Uingereza upo Tanzania kwa ajili ya kutafuta fursa za biashara.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam ujumbe umeeleza kuwa unalenga kutambua na kutumia fursa mpya ya kibiashara, ukiwa ni ujumbe wa kwanza kufanya hivyo chini ya mwavuli wa UK Trade and Investment - taasisi ya uwekezaji kutoka Uingereza.
Kiongozi wa ujumbe huo David Billingsby amesema Tanzania kama mojawapo ya mataifa ya Afrika yenye uchumi unaokua kwa kasi Afrika ina mazingira muafaka ya kuwekeza ambayo makampuni ya kiingereza yameona ni vizuri kufanyia utafiti.
Alipoulizwa endapo kazi hiyo ni sehemu ya mpango wa nchi za magharibu kutaka kupunguza misaada na kuelekeza nguvu katika biashara ya pande mbili Bwana Billingsby alieleza kuwa vyote viwili misaada na biashara vinatakiwa kufanya kazi kwa pamoja kuwezesha ukuaji wa uchumi na kupatikana kwa ajira.
Baadhi ya makampuni katika ujumbe huo ni Eagle Scientific, thp Machine Tools na Concept Smoke Screen.
Siku ya Alhamisi watakutaka na viongozi wa biashara nchini Tanzania kujadili moja kwa moja maswala na fursa za kibiashara.
Makampuni mengi zaidi ya Kiingereza yanaweza kujitokeza katika biashara za mafuta na gesi yaliyogunduliwa kusini mwa Tanzania na tayari kampuni kubwa kama BG inashiriki katika mpango wa kujenga mtambo wa kusafirisha gesi kwenda nje.
Next Post Previous Post
Bukobawadau