Bukobawadau

SIKU YA MWALIMU DUNIANI KITAIFA MKOANI KAGERA LEO 5/10/2014 ;Walimu Kuundiwa Tume ya Utumishi Wao na Bodi ya Fani ya Ualimu ifikapo 2015

WAZIRI MKUU PINDA ASEMA SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA WATUMISHI WALIOHAKIKI MADENI HEWA YA WALIMU NA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA
·         Walimu Kuundiwa Tume ya Utumishi Wao na Bodi ya Fani ya Ualimu ifikapo 2015
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amesema serikali itawashughulikia watumishi wasiokuwa waadilifu waliohakiki madeni ya walimu nchini na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 10 kwa kuwasilisha madeni yasiyokuwa ya kweli kwa manufaa yao binafsi.
Waziri Mkuu Pinda aliyasema hayo wakati akihutubia taifa kwa ujumla kwenye  maadhimisho ya  Siku ya Mwalimu Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Kagera Jumapili Octoba 5, 2014 katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba.
Waziri Mkuu alisema kuwa serikali itachukua hatua kali kwa watendaji walioisababishia hasara serikali kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe binafsi kupitia madai ya walimu nchini  wakati akijibu risara ya walimu iliyosomwa mbele yake na  Mwalimu Yahya Msulwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
 Katika risara ya walimu waliiomba serikali kuyafanyia kazi kwa uharaka mambo makuu muhimu kumi na moja, ikiwa moja ni Upandishwaji wa Madaraja kwa walimu kwa wakati, Pili ni Mishahara midogo kwa walimu huku wakifanya kazi zaidi na mishara maalumu kwa wakuu wa taasisi kama wakuu wa shule na waratibu na Maafisa Elimu.
Tatu, madeni ya walimu kulipwa kwa wakati, nne ni uhaba wa nyumba za walimu, tano ni mchakato wa utoaji  elimu bora nchini, vyou kudaili wanafunzi wa fani ya ualimu wenye vigezo kama fani nyinginezo, sita  ni kuhusu janga la UKIMWI kwa walimu, Saba ni kuhusu serikali kuunda chombo kimoja cha ajira na Huduma kwa walimu.
 Nane, ni mabadiliko ya mafao ya Pensheni kwa walimu kwa kutumia kanuni mpya ya SSRA, jambo la tisa ni kuhusu kuboresha idara ya ukaguzi wa shule, kumi ni mpango wa Matokeo Makubwa sasa kuihusisha elimu kwa raslimali fedha na raslimali watu. Mwisho ni kuhusu ukosefu wa umakini kwa baadhi ya watendaji wa wanaohudumia walimu katika ngazi za Wizara na Halamashauri
Waziri Mkuu Pinda akijibu hoja hizo alisema serikali inaendelea kuzitatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu nchini lakini akasema matatizo hayo yanatokana na kuongezeka kwa huduma za elimu nchini pia ikiendana na ongezeko la walimu wanaoongezeka kulingana na mahitaji katika sekta ya  elimu.
Mhe.  Pinda alisema mwaka 1961 wananfunzi wa shule za msingi walikuwa 486,470 na waliongezeka hadi 8,419,305 mwaka 2010 sawa na ongezeko la wastani wa wanafunzi 149, 676.1 kwa mwaka. Shule za Msingi zimeongezeka kutoka 3,000mwaka 1961 hadi 15,816 mwaka 2010 sawa na ongezeko la shule 241.8 kila mwaka.
Aidha idadi ya walimu imeongezeka kutoka 9,885 mwaka 1961 hadi 165,856 mwaka 2010 sawa  na wastani wa ongezeko la walimu 2,942.8  kwa mwaka. Pia madarasa yameongezeka kutoka  3,100 mwaka 1961hadi 110,342 mwaka 2010 sawa na wastani wa ongezeko la madarasa 2,023.4 kila mwaka .
Waziri Mkuu pia alisema matatizo mengi ya walimu yanasababishwa na kutotumia TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ) katika kushughulikia masuala mbalimbali yanayowahusu walimu na ndiyo maana kero nyingi zinajitokeza mara kwa mara lakini serikali imejipanga kulishughulikia tatizo hilo.
Vilevile Waziri Pinda akijibu risara ya walimu nchini alisema kuwa serikali tayari imekubaliana na ukweli kuwa utumishi wa walimu ni zaidi ya asilimia 50 ya watumishi wote nchini kwa hiyo tayari serkali imekubali kuunda Tume ya Utumishi wa wa limu (Teachers Service Commission) ili kushughulikia masuala ya walimu.
Aidha  serikali itaunda chombo kama Bodi ya walimu ili kuifanya fani ya ualimu kutambulika kama fani zingine nchini alisistiza Waziri Mkuu, ikiwa ni pamoja kuiunda upya TSD na kuiwezesha idara ya ukaguzi wa shule kukidhi viwango katika kuimarisha elimu nchini.
Serikali pia inaangalia uwezekano wa kuingia ubia na mashirika binafsi kuona kama itatatua tatizo la nyumba za walimu ili walimu wapate makazi bora. Pia serikali imeunda shirika jipa Watumishi Housing ili kuhakikisha watumishi wa umma wanapata makazi bora kwa kujenga nyumba zao wenyewe kwa mikopo nafuu kutoka Watumishi Haousing. Alisistiza kuhusu juhudi za serikali Mhe. Pinda.
Akihitimisha hotuba yake Waziri Mkuu Pinda alisema kuhusu ukosefu wa umakini kwa baadhi ya watendaji wanaohudumia walimu katika ngazi za Wizara na Halamashauri limekuwa ni tatizo kubwa nchini kwani watendaji wengine wanankuwa na roho mbaya bila sababu na kukataa kusikiliza shida za walimu lakini serikali inapobaini hushughulikia suala hilo mara moja.
Siku ya Mwalimu Duniani huadhimishwa tarehe 05 Oktoba kila mwaka.  Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu yalianzishwa rasmi na Shirikisho la Walimu Duniani (EI) mwaka 1993. Kwa Tanzania maadhimisho ya Siku ya Mwalimu ni mara ya tatu kuadhimishwa mwaka 2006 yalifanyika Mkoani Mtwara, mwaka 2010 yalifanyika mkoani Ruvuma na Mwaka huu 2014 mkoani Kagera.
Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani hufanyika kila baada ya miaka mitatu aidha kaulimbiu ya Mwaka huu ilikuwa nia “Invest in the future/Invest in Teachers maana yake kwa tafsiri ni Wekeza kwa maisha ya baadae/Wekeza kwa Mwalimu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau