12 November 2014
AJALI MBAYA KAHAMA MAPEMA YA LEO
Bus laWibonela (Kahama-Dar) limepata ajali huko Kahama leo asubuhi,maeneo ya Phantom
Kibaka aliyekuwa anapekua na kuchomoa fedha na Vitu kwa majeruhi wa ajali apigwa na kuchomwa moto
Hadi kufikia sasa haijajulikana majeruhi ni wangapi na waliokufa ni wangapi
Picha kwa hisani ya Rafiki Prince kutoka eneo la tukio
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comment:
Jamani ooooh M.Mungu nini jamani kila siku vilio nchini kwetu, kweli hizi ajali zimezidi kweli ni tatizo la Leseni? ama!!! ninawasiwasi sana na Leseni nchini kwangu, watu wanakufa bila hatia jamani, tuangalieni sana nchi yetu, nchi ya amani, tumeepuka mengi mojawapo gonjwa la Ebola sasa inakuaje tusijiwekee misingi ya kulinda uhai wa ndugu zetu? jamani! ukiuliza nini chanzo wanasema speed!! Mungu ziweke roho za marehemu mahala pema pepo, nawaponye haraka walopana katika hajari hiyo.
speed speeed.Maviii h.k Germany
Nilisema kwamba kinachotumaliza ni trafiki na si ajali mdau mmoja akasema nisiende huko, eti mbona hata ndege zinaanguka kwani nazo ni trafiki! Ni kwamba ukifanyika uhakiki wa uhakika sidhani kama unaweza kupata hata dreva mmoja kati ya 10 mwenye leseni ya kweli kwa hawa wanaoendesha magari makubwa ya abiria. Wengi wamejifunzia kuendesha kwenye karakana za magari, wakitoka hapo wanafanya wanavyojua na kupata leseni. Kusema ukweli hawaelewi lolote kuhusu sheria za barabarani. Siku moja nilikoswakoswa na basi liendalo mikoani nikiwa na askari wa usalama barabarani kwenye kivuko cha pundamilia, ajabu hata askari huyo hakuona kama pale kuna hitilafu! Yeye ndiye aliyeniambia, "I say tumeponea chupuchupu"! Kwa mtindo huo ajali ikitokea niseme ni ajali au trafiki?
Post a Comment