Bukobawadau

BURIANI KAMANDA STIVIN LEONARD MTENSA

Buriani Kamanda Mtensa!  Mpendwa wa wana Bukoba hayati Leonard Mutensa alitutoka ghafla mwanzoni mwa wiki iliyopita na jana Jumamosi, tarehe 22 Novemba, 2014 wana Bukoba waliungana na familia ya marehemu kwenye mazishi ambayo hayana ubishi ya kudhihirisha ukweli marehemu alikuwa ni kipenzi cha wana Bukoba. Mazishi ya Mtensa, yalidhihirisha Mutensa alikuwa ni Kamanda wa maendeleo ya jamii na uchumi ya Bukoba.
Marehemu Stivin Leonard Mtensa ,hapa ndipo alipo pumzishwa katika Nyumba yake ya Milele  tumuombee kwa Mwenyezi Mungu alaze roho yake pema peponi, Apumzike kwa amani
 Shughuli nzima ya mazishi ya Mutensa ilianza siku ya Ijumaa mwili wake ulipochukuliwa kutoka Chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa, iliyopo Bukoba mjini. Kulikuwepo na umati mkubwa wa waombolezaji wakiwemo watu mashuhuri wa Bukoba na wengine wengi kutoka mikoa mingine ya Tanzania kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza. Waombolezaji wengine walitokea nchi Jirani kama Uganda na Rwanda. Mchanganyiko wa waomboleza hi unadhihirisha jinsi Mtensa alivyokuwa amejipanua na kujenga mahusiano ya kibiashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Madhariki.
 Familia inapenda kutanguliza Shukrani zake za dhati kwa jinsi mlivyojitolea kufanikisha safari ya Mwisho  ya Marehemu Stivin Leonard Mtensa,Shukrani kwa 1. Kamati ya msiba 2.Madaktari
 3.Shukrani kwa Polisi 4.Viongozi wa Dini 5.Pamoja group 6. Ndugu, jamaa na marafiki ambao kwa namna yoyote wameshiriki katika hili na lile.
Familia inatoa shukrani za pekee kwa 1. Pamoja Group 2.Mr. Alphonce Inocent (Pajero) 3 Mr. Fortunatus Kajuna 4. Mwalimu Jackson Buberwa 5. Mr. Kaloli kutoka Mtukula 6.Mr Rahym Kabyemela 7.Self Mkude 8. Familia ya Kichwabuta ikiongozwa na Majidi na Jeanifer 9. Ndugu Allanus Kasharaba ( Dar es Salaam) 10. Mr.Justuce Rugaibura na Ben Kataruga (Dar es Salaam)
 Shukrani za kipekee kwa Kaka Mkubwa E. Nyambo,hakuna maneno sahihi tunayoweza kutumia kueleza shukrani zetu zaidi tuunakuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kukupa afya njema, hekima na busara zaidi wahaya wanasema 'Ogume Obeileo'

Kutoka Chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya mkoa, mwili  wa marehemu Mtensa uliwekwa juu ya Gari la wazi ambalo lilipita nje ya Klabu yake ya Lina's na kuzunguka kupitia Mtaa maarufu wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba.
 Mji wa Bukoba na viunga vyake umeendelea kuzizima jioni ya hiyo kutokana na msiba huu, Katika hatua nyingine, vilio na simanzi vilitanda kila kona lilipopitishwa jeneza lenye mwili wa Marehemu Mutensa Leonard.
 Maeneo yote ulikopitishwa mwili wa Mutensa, shughuli zote zilisimama na watu walidhihirisha kuwa katika majonzi makubwa kwa kuondokewa na Kamanda, muwekezaji ambaye Biashara zake zinahusika na kutoa ajira kwa watu wasiopungua Mia moja hapa mjini Bukoba.
.Ni dhahiri tukichukua kigezo cha ajira, kifo cha Mutensa kitaleta mtikisiko katika maendeleo ya jamii na uchumi wa Bukoba. Ni jambo linalojulikana dhahiri kwamba yeye ndiye aliyekuwa mhimili wa Biashara zake zote. Kuondoka kwake kwa kifo cha ghafla, itaichukuwa familia yake muda kidogo kujipanga upya ili kusogeza mbele majukumu yote ya Biashara za Mutensa kwa ufanisi. Itakuwa ni kwa kudra za Mwenyezi Mungu, katika kipindi cha mpito pasitokee madhara kama baadhi ya wafanyakazi kupunguzwa Kazi.
 Ndugu Saimon Desare mmoja kati ya marafiki wa karibu na marehemu Mtensa Leonard
Taswira mbalimbali eneo la tukio
Ni majonzi kwa kila aliyemjua Marehemu Mtensa Leonard
 
 Kushoto ni Mama Mzazi wa Mjane wa Marehemu muda mchache kabla ya Misa maalum kuanza.
 Mr. Peter Mgisha katika hali ya huzuni ,pembeni yake ni Hajj Kambuga mmoja wa wazee wa familia
Vijana wa  kikosi kazi maalum wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mtensa Leonard  kutoka ndani ya Nyumba  kuelekea Ukumbini kwa ajili ya Misa ya Mazishi iliyohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka Nje na Ndani ya nchi.
 Front line yupo Rahym Kabyemela na Jamal Kalumuna.

 Vijana Smart wakiwa kwenye vazi  aina ya suti wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mtensa Leonard aliyefariki hivi karibuni kwa kifo cha ghafla ambapo mpaka sasa chanzo cha kifo  hicho bado hakijajulikana 
Wanatembea kwa mwendo wa pole pole wakati wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu  Mtensa Leonard.
 Mjane wa Marehemu Mtensa Leonard.
 Pichani Kushoto ni Mzee Rugaibura
 Pole sana Benna pole sana Mama Deo  pole kwako mama Prince.
 Pichani ni  watoto watatu kati yawatano wa kuzaliwa na Marehemu Mtensa Leonard.
 Mzee Rugaibura, Mzee Frank Theophi na Mzee Mchuruza wakiendelea na Misa ya mazishi. 
 Pichani Katikati anaonekana Mr. Karoli wa Mutukula, huyu ni mmoja wa wafanyabiashara maarufu kwa ukanda wetu waliotokea kupatapa mafanikio makubwa kupitia  mikononi mwa Marehemu Mtensa Leonard ambaye leo Jumamosi Nov 22,tunampumzisha katika makazi yake ya milele
 Bi Letty akiendelea na misa hii maalum kumuaga Mpambanaji, mzalendo Marehemu Mtensa
 Katika sintofahamu anaonekana Bi Anitha David Mtensa.
 Shughuli ya Misa ikiendelea,hapa kikubwa ni mpangilio wa shughuli nzima,heshima kubwa kwa mwili wa Marehemu sanjari na Wingi wa watu ni hali iliyoongeza mazishi hayo kuwa ya aina yake.
 Mr. Ben Kataruga na Mr Justuce Rugaibura wakiwa wametoka Jijini Dar es Salaam kushiriki  shughuli ya mazishi ya Rafiki yao , Kaka yao mpendwa Marehemu Mtensa Leonard
Sehemu ya Wanakwaya.
 Mzee Baganda na Mzee Nyerere waliokaa mstari wa mbele.
Umati mkubwa wa watu  wakiendelea kushiriki Misa ya shughuli ya Mazishi ya Marehemu Mtensa Leonard nyumbani kwake Kyaikailabwa  takribani kilomita 3 nje kidogo ya Mji wa Bukoba
 Sehemu ya wanachama wapambanaji 'Wanapamoja' wakiendelea kushiriki  Misa ya kumuaga  Ndugu yao, rafiki yao ,kaka yao mpendwa na  mwanachama mwenzao mtu wa watu Marehemu Mtensa Leonard.
 Kutoka kushoto ni Mzee Baganda akifuatiwa na Mzee Philbart Nyerere na Mzee Pius Ngeze
 Mdau Yusuph Abed (Dj Y) na  (Dj Ray )hakika wameguswa sana na msiba huu.
Inasikitisha na kuhuzunisha ,pichani kushoto ni Mama Mzazi  wa Mjane wa Marehemu akiwa na  (Ma Kossi)ambaye ni Mama Mzazi wa Marehemu Mtensa kwa pamoja wanamlilia mpendwa wao
 Kutoka kushoto ni Jamal (Jamco)Kalumuna, Rahym Kabyemela, Mc Baraka (Bukobawadau), Ndg Rmk Ramadhani Maulid Kambuga Mr. Follo , Gilbart Gsmart George na  Ndg Samola Lyakurwa.
 Mr. Innocent Pajero , Mc Jerry na Ndugu Optaty Folo pichani.
 Kaka Mkubwa E.Nyambo anamwongoza Mama Mzazi wa Marehemu Leonard Mtensa kushuhudia.
 Bi Benna Kurji Mrs Deo ambaye ni shemeji ya Marehemu Leonard Mtensa
 Jeanifer Murungi KichwabutaWatoto wa Marehemu wakitoa heshima za mwisho..'Tutakukumbuka Baba yetu mpendwa'!
Watoto J mmoja wa marehemu wakiaga mwili wa baba yao huku wakilia kwa uchungu
Katika zoezi la kushuhudia anaonekana Mzee Yusto Mchuruza.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Ben Expeditions akitoa heshima za mwisho.
Mkubwa Justuce Rugaibura kutoka Jijini Dar es Salaam akitoa heshima zake za mwisho
 Mama Muhazi, rafiki wa familia akishiriki zoezi la kutoa heshima za mwisho
 Kaka Mkubwa Ernest Nyambo akitoa heshima za mwisho kwa rafiki yake,'katikilo wake' Mtensa
 Watu mbalimbali wakiendelea kuhushu
 Mh. Yusuph Ngaiza Diwani Kata Kashai mara baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake
 Mtawa wa kanisa Katoliki nchini akitoa heshima zake za mwisho kuuaga mwili wa Marehemu
 Mrs David Mtensa
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Linas Club wakitoa heshima za mwisho
 Zoezi la kutoa heshima za mwisho likiendelea
 Mr.Minas Visram na Mr. Bandali wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa rafiki yao
 Waombelezaji wakiendelea kutoa  heshima za mwisho
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa ,ni hakika kifo cha Mtensa ni huzuni mkubwa
 Mzee Ojwambo katika zoezi la  kushuhudia.
Mzee Pius Ngeze  akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu
 The futuhi....
 Ndugu Phibart akishuhudia Mwili wa rafiki yake mpendwa Stivin Leonard Mtensa
 Mzee Salum Chama Umande
 Uncle Salum na Mr Deo wakiteta jambo
Shukrani za pekee kwako Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta Bukobawadau tumeshuhudia namna  ulivyojitoa kwa nguvu zako zote kwa hali na mali  katika msiba huu .

 Mama Petel Mulima pichani
 Wadau wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Mpambanaji Marehemu Mtensa.
 Mr. Deo Rugaibura, Uncle Salum na Ndg Optaty Kajuna (Follo)
 Mama Mwainunu akitoa neno na rambirambi kwa niaba ya 'Wanapamoja'
 Kaka Mkubwa Ernest Nyambo akitoa yake ya moyoni kwa niaba yake binafsi na kufikisha kile kilichotoka kwa Bukoba Veterans katika kusupport msiba huu mkubwa wa mwenzao.
 Waakirishi kutoka Kikundi cha Sanaa cha Futuhi wakiongozwa na Mdau Mzalendo Willy Kiroyera
Kutoka kundi maarufu la Futuhi la jijini Mwanza wameguswa sana na msiba huu 'Ebyehatari'!
 Mwalimu Bube, ambaye ndiye aliyekukuwa swahiba wa karibu na Marehemu anatoa utambulisho kwa watoto wa Marehemu kabla ya kusoma wasifu wake.
 Marehemu Mtensa Leonard ameacha Mjane na watoto wa tano,Wanne wa Kiume na Mmoja wa Kike, pichani ndiye  kitinda mimba kwa jina ni Stalon Mtensa.
Mr.Alfred Matovelo akiwa ametoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki mazishi ya rafiki yake
  Watu wanalia! wanahudhunika na machozi yanawatoka kufuatia msiba huu wa kihistoria.
Bi Linna Mtensa  mtoto mkubwa wa Marehemu Mtensa Leonard
 Katika Utayari kuubeba Mwili wa Marehemu Mtensa Leonard Kuelekea eneo la Kaburi
 Kuelekea eneo la Kaburi
Umati wa watu  ukiweka mikono hewani  yenye maua mazuri ikiwa ni Ishara ya upendo  wakati jeneza likiwa limebebwa kuelekea eneo la Kaburi
 Wakati tukiendelea tunapokea Salaam za rambirambi kutoka kwa Ndg  Bennett Rweyemamu akiwa Dar es Salaam,anasema;'Nakumbuka mara ya mwisho kabisa miaka miwili nikiwa Bukoba Kaka Mtensa ndo alikuwa mtu wa mwisho kuachana naye, tumeachana karibuni saa saba usiku nikiwa na mdogo wake Mugisha na kesho yake nikapanda ndege kuelekea Dar es Salaam. Kwa kweli usiku ule nilifarijika sana sana kwa kuwa kwangu na Kaka Mtensa kwani tukiongea mengi sana na kanipa maneno makubwa sana kanizungusha kwenye miradi yake yooote na nikamuahidi tungeshirikiana pale ambapo tungeweza kuhitajiana'
 Kusema ukweli. Ni majonzi makubwa sana, sana kumpoteza mpiganaji mzalendo wa mkoa wa Kagera na mji wa Bukoba kwa ujumla. Kwa heshima zote nawatakia ndugu, familia, marafiki na jamaa wote moyo wa Subra kwa kupoteza JEMBE!!!!! Mungu akupokee Kaka Mtensa! Amen. (Bennett Rweyemamu-Dar es Salaam)
 Naam! Kikosi kazi kwa mwendo wa pole pole wakati wamebeba jeneza lenye mwili wa Mpambanaji, Kamanda Mtensa jamani ile hali nyuma yao maua ya watu yapo hewani
  Tazamahali ya majonzi ilivyo kubwa sana,Mwalimu Bube  pichani ni kipimo namna watu walivyoguswa na Mtensa
Watoto wa Marehemu wakiongozana na Kikosi kazi sambamba na ndugu wa familia
 Salute kwao Smart Boys aka Kikosi Kazi kwa tukio hili hakika Dunia imesimama kwa muda, Macho na masikio kokote pale yapo Bukoba, kikubwa ni shughuli ya mazishi ya Jemedali  Mtensa
 Mwanzo wa Safari ya Mwisho ya Uhai wa maisha ya Duniani kwa Mpambanaji Mtensa
Daahh 'Mtensa yagenda' raha ya milele ikuangazie mkurugenzi!
 Jeneza likiingizwa Kaburini
Mama Mjane akiweka Udongo kwenye Kaburi la mme wake Mpendwa.
 Mwalimu Jackson Buberwa akiweka Udongo kwenye kaburi
Mrs Deo Rugaibura, akiweka Udongo kaburini
 Ndugu wa Familia, Ndg David na Ndugu Mgisha wakiwa tayari kuweka Udongo kwenye kaburi
Kwa siku ya Jana Ndugu Ernest Nyambo alisema: 'Faraja yangu imekuja pale nilipo MZIKA rafiki yangu kwa style niliyotaka,kwa heshima kubwa,kwa mpangilio THABITI,sherehe yako ya mwisho kaka Mtensa ilikuwa KALI SANA,USHINDI WA MANCHESTER UNITED JANA KWA ARSENAL NI USHINDI WAKO BROTHER,nakupenda sana MPAMBANAJI Leonard Mtensa
 Mama Mzazi wa Marehemu tayari kwa ajili ya kuweka shada la maua.
 Mjane Mama Linna anaweka Shada la maua katika kaburi la Marehemu mme wake
 Binti wa Marehemu Mtensa Leonard akiweka shada la maua
 Ndugu Optaty Kajuna anaweka shada la Maua.
 Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea.
Mr . Ben Kataruga na Mwenzake Justuce Rugaibura wakiweka shada la maua
 Kwa umahiri mkubwa Mr. Bube akielezea anavyomfahamu marehemu nje ndani anasema; Marehemu  Mtensa katika kuwepo kwake Duniani alipenda sana wimbo uitwao(I Will Always Love You wa Whitney Houston)hivyo anahakika wimbo huo ukipigwa mahali hapa tutakuwa tumetenda haki kwa Marehemu Mtensa Leonard


 Mr. Bube akiendelea kutolea jambo ufafanuzi
 Neno kutoka kwa Hajj Maulid Kambuga kwa niaba ya Wazee.
Sehemu ya waombolezaji
 Neno la Shukrani kwa wato walioshiriki shughuli ya kumuaga Mpendwa wetu linatolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Mazishi Ndugu Self (Super) Mkude
 Mc Muongozaji akitoa utaratibu
 Anaitwa Linna, mtoto mkubwa au wa kwanza kuzaliwa na Marehemu Leonard Mtensa
Marabaada yashughuli nzima ya mazishi.
 Ndivyo linavyo onekana kaburi la Marehemu S.Leonard Mtensa likiwa na maua kila aina
 Mara baada ya Shughuli ya Mazishiwadau wakibadirishana mawazo
 Washirika wa Bukoba Veterans,Shukrani kubwa kwenu kwa niaba ya familia ya Marehemu
Mh.Rwaks  Wilfred Lwakatareameweza kushiriki katika maziko haya.
 Kikosi kazi maalum katika picha ya kumbukumbu
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Linas Night Club.
Rais wa COSAD Tanzani Ndg Smart Baitani
 Marehemu Mtensa alikuwa ni mpambanaji aliyejitahidi kuibadilisha Bukoba kwa jitihada za ujasitiamali. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Bukoba ambao kwao Bukoba ilikuwa ni kila kitu, kuwekeza Bukoba kuna changamoto nyingi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe. Tumuombe Mungu aipokee roho ya marehemu na ampatie pumziko la amani.
 Marehemu Mtensa alikuwa ni mpambanaji aliyejitahidi kuibadilisha Bukoba kwa jitihada za ujasitiamali. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Bukoba ambao kwao Bukoba ilikuwa ni kila kitu, kuwekeza Bukoba kuna changamoto nyingi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe. Tumuombe Mungu aipokee roho ya marehemu na ampatie pumziko la amani.
 Kwa matukio ya picha zaidi ya 200 unaweza  kujiunga nasi katika Ukurasa wetu wa facebook kupitia link hii hapa>> Bukobawadau Entertainment Media Next Post Previous Post
Bukobawadau